Pata taarifa kuu

Mfahamu Mikhail Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa enzi ya vita

Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Urusi, alishiriki pakubwa katika mikataba kati ya Muungano wa Usovieti na Marekani ya kutaka kupunguza silaha, na ushirikiano na madola ya Magharibi ili kuondoa wingu nzito la mgawanyiko wa Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia na kupelekea muungano wa Ujerumani. Lakini mageuzi yake mapana ya ndani yalisaidia kudhoofisha Umoja wa Kisovieti hadi ikasambaratika, muda ambao Rais Vladimir Putin ameuita "janga kubwa zaidi la kisiasa la kijiografia" la karne ya ishirini.

Mmoja wa watu wakuu wa kisiasa wa karne ya 20, Mikhail Gorbachev aliaga dunia Jumanne Agosti 30 akiwa na umri wa miaka 91 huko Moscow.
Mmoja wa watu wakuu wa kisiasa wa karne ya 20, Mikhail Gorbachev aliaga dunia Jumanne Agosti 30 akiwa na umri wa miaka 91 huko Moscow. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

 

Mikhail Gorbachev, aliyezaliwa Machi 2, 1931 katika kijiji cha Privolnoïe, Caucasus Kaskazini, katika eneo ambalo sasa linaitwa Stavropol, alipenda kusema kwamba alikuwa dereva wa mavuno. Kwa kweli, mtoto na mjukuu wa wakulima, alichanganya masomo yake na kazi za mashambani kusaidia baba yake huko kolkhoz.

Atakumbukwa kwa mchango wake wa kumaliza vita baridi bila umwagaji damu lakini akikosolewa kwa kushindwa kuzuia kusambaratika kwa Umoja wa kisovieti. 

Mnamo tarehe 25 Desemba mwaka 1991, Gorbachev aliyekuwa ameuongoza Umoja wa Kisovieti kwa miaka saba alijiuzulu wadhifa wake, na bendera ya muungano huo ilishushwa na kupandishwa ile shirikisho la Urusi. Kuanzia mwaka 1985 hadi kuanguka kwa muungano huo mwaka 1991, Gorbachev alisimamia mageuzi makubwa ya sera za kiuchumi na kisiasa za Urusi.

Mikhail Gorbachev alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika siasa karne ya 20.

Aliongoza kuvunjwa kwa Muungano wa Sovieti ambao ulikuwepo kwa karibu miaka 70 na ulikuwa umetawala sehemu kubwa za Asia na Ulaya Mashariki.

Hata hivyo, alipoanzisha mpango wake wa mageuzi mwaka 1985, nia yake pekee ilikuwa ni kufufua uchumi wa nchi yake uliodumaa na kurekebisha michakato yake ya kisiasa.

Juhudi zake zikawa kichocheo cha mfululizo wa matukio ambayo yalileta mwisho wa utawala wa kikomunisti, sio tu ndani ya USSR, lakini pia katika mataifa mengine.

Alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1990 kwa kusaini mkataba wa kihistoria wa silaha za nyuklia na kiongozi wa Marekani wa wakati huo Ronald Reagan.

Viongozi wa dunia wamkumbuka

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha kiongozi huyo. Salamu za pole pia zimetolewa na rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, aliyemuelezea kiongozi huyo kuwa "mtu mwenye mchango muhimu katika kumalizwa kwa vita baridi na aliyeondoa uhasama baina ya umoja wa kisovieti na nchi za magharibi, hatua iliyofungua njia ya "ulaya huru". Vita Baridi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika salamu zake za pole, amemsifu Gorbachev, kama "kiongozi wa kipekee aliyeibadilisha dunia kuwa bora". Amesema Gorbachev ni "mwanasiasa wa aina yake ambaye alibadilisha mkondo wa historia. Viongozi wengine waliotuma salamu za pole ni pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakimwelezea kuwa "mtu wa amani" aliyeonesha "uadilifu na ujasiri".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.