Pata taarifa kuu

Urusi yaishutumu Ukraine kwa kumuua binti wa mwanafalsafa Alexander Dugin

Idara za usalama za Urusi zimetangaza hadharani hitimisho la uchunguzi wao. Kulingana na FSB mnamo Jumatatu, Agosti 22, mauaji haya "yalipangwa na kufanywa na idara maalum za Ukraine".

Mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya siasa Daria Douguina, hapa kwenye akitangaza moja kwa moka kwenye kituo cha Tsargrad, huko Moscow, Agosti 21, 2022.
Mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya siasa Daria Douguina, hapa kwenye akitangaza moja kwa moka kwenye kituo cha Tsargrad, huko Moscow, Agosti 21, 2022. via REUTERS - TSARGRAD.TV
Matangazo ya kibiashara

Idara za usalama za Urusi, FSB, zimetangaza matokeo ya uchunguzi wao kwa umma. Idara za usalama za Urusi zimemtaja mwanamke aliyetekeleza mauaji ya Daria Douguina: raia wa Ukraine aliyezaliwa mwaka wa 1979 na ambaye amekimbilia nchini Estonia baada ya kutekeleza uhalifu. Mwanamke huyu, kulingana na FSB, alifika nchini Urusi akiambatana na binti yake mnamo Julai 23 na wote walikuwepo kwenye tamasha katika vitongoji vya Moscow ambapo mwathirika alikuwa mgeni wa heshima siku ya mauaji.

Wakati huohuo, washtakiwa hao wawili walikodisha chumba katika ghorofa huko Moscow katika nyumba ambayo Daria Douguina alikwa akiishi, waliwalimfuatialia kwa karibu popote pale alipokuwa akienda kwa kutumia gari ilikuwa na nambari tatu tofauti za usajili: moja ya Jamhuri ya kujitenga inayounga mkono Urusi ya Donetsk. alipoingia Urusi, nyingine kutoka Kazakhstan alipokuwa akitafutwa huko Moscow, kisha ya mwisho kutoka Ukraine aliondoka nchini Urusi.

Ama mauaji yaliyoelezewa kuwa "yalipangwa na kuamriwa na idara maalum za Ukraine". Jukumu hili la Kyiv lilitajwa Jumapili Agosti 21 asubuhi na sauti nyingi nchini Urusi, ikiwa ni pamoja na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje.

 

► Soma pia: Urusi: Binti wa mshirika wa karibu wa Putin auawa katika mlipuko wa gari lake

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.