Pata taarifa kuu

Taiwan yaikosoa China kwa kuendeleza mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho

Taiwan siku ya Jumatatu imeilaumu China kwa kufanya mazoezi mapya ya kijeshi ya baharini na angani karibu na kisiwa hicho, huku Beijing ikiendelea kulipiza kisasi kufuatia ziara ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi.Β 

Helikopta za kijeshi za China zinaruka juu ya Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika jimbo la Fujian mnamo Agosti 4, 2022, kabla ya mazoezi makubwa ya kijeshi kwenye pwani Taiwan.
Helikopta za kijeshi za China zinaruka juu ya Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika jimbo la Fujian mnamo Agosti 4, 2022, kabla ya mazoezi makubwa ya kijeshi kwenye pwani Taiwan. AFP - HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

"Wizara ya Mambo ya Nje inalaani vikali uamuzi wa China wa kuongeza muda wa mazoezi ya kijeshi. Uchokozi na uvamizi wa China umedhoofisha hali ya sasa katika Mlango wa Bahari wa Taiwan na kuibua mvutano katika eneo hilo," amesema katika taarifa yake.

Mazoezi haya, angalau katika usanidi huu, yalipaswa kumalizika Jumapili mchana (saa moja asubuhi saa za Afrika Mashariki) kulingana na idara ya usalama wa baharini nchini China. Lakini mazoezi haya yanaendelea Jumatatu. "Jeshi la Ukombozi la Watu...linaendelea kufanya mazoezi ya pamoja ya anga na baharini kwa kuzunguka Taiwan, kwa kuzingatia operesheni za pamoja za kupambana na manowari na mashambulizi ya baharini," makao makuu ya jeshi katika eneo la Mashariki limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alikuwa ameshutumu "kutokuwa na uwiano kamili" juu ya hatua ya China na hasa ya kuanzisha mazoezi haya, wakati ambapo makombora ya China yalirushwa. Baada ya kukosolewa na kundi la nchi zilizoshtawi kiuchumi, G7 na Marekani, alitoa taarifa ya pamoja na wenzake wa Japan na Australia akitoa wito kwa China kusitisha mazoezi haya ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.