Pata taarifa kuu
Japani - Siasa

Japan : Waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe amefariki

Waziri mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, amefariki baada ya kupigwa risasi mapema leo kwenye mkutano wa kampeini, kutuo cha habari cha serikali nchini Japan, kimeripoti .

Shinzo Abe, alikuwa waziri mkuu wa Japan.
Shinzo Abe, alikuwa waziri mkuu wa Japan. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Abe aliyekuwa na umri wa 67, alikuwa waziri mkuu wa Japan ambaye alihudumu kwa muda mrefu hadi kujiuzulu kwake mwaka 2020, alipigwa risasi wakati akitoa hutuba kwenye mkutano wa kampeini.

Abe alipigwa risasi mara mbili wakati akitoa hutuba katika jiji la Nara, kusini mwa Japan, ambapo alizimia na kukimbizwa hospitalini.

Waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida, akiwa amejawa na majonzi, amelaani kitendo hicho na kukitaja kuwa cha kioga mbacho kamwe hakiwezi kuruhusiwa nchini Japan.

Mshukiwa wa mauwaji hayo tayari mwanaume wa miaka 40, amekamatwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.