Pata taarifa kuu

Malaysia yakumbwa na maandamano dhidi ya ufisadi

Mamia ya watu wamekusanyika Jumamosi hii mjini Kuala Lumpur kumtaka kiongozi wa shirika la kupambana na rushwa nchini Malaysia, kiongozi mwenye ushawishi, Azam Baki, kujiuzulu kwa kuhusishwa na biashara ya hisa iliyozua utata ambapo alikuwa anamiliki mamilioni ya hisa.

Kuala Lumpur, Januari 22, 2022: Maandamano dhidi ya ufisadi. Katika bango hilo, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (MACC), Azam Baki, anashukiwa kuwa na hisa nyingi kuliko inavyoruhusiwa na sheria za Malaysia.
Kuala Lumpur, Januari 22, 2022: Maandamano dhidi ya ufisadi. Katika bango hilo, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (MACC), Azam Baki, anashukiwa kuwa na hisa nyingi kuliko inavyoruhusiwa na sheria za Malaysia. AFP - ARIF KARTONO
Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyu wa shirika la kupambana na ufisadi (MACC) alikiri kununua mwaka wa 2015 baadhi ya euro 210,000 za hisa za kampuni mbili zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa kwa kutumia akaunti yake ya biashara. Hata hivyo, sheria inakataza maafisa wa umma kumiliki zaidi ya RM 100,000 kutoka kwa kampuni, ameripoti mwandishi wetu wa Kuala Lumpur. Azam Baki amejitetea kwa kusema alifanya kwa niaba ya kaka yake jambo ambalo shirika la soko la hisa la Malaysia limekanusha.

Wakiwa wamevalia barakoa na kupiga kelele wakisema "tunakataa rushwa", baadhi ya waandamanaji 200, wengi wao wakiwa wamevalia nguo nyeusi, walitoa wito kwa Azam Baki, afisa wa ngazi ya juu wa taasisi ya kupambana na rushwa (MACC) kuchukuliwa hatua.

Tangu kuanza kwa janga la Covid, maandamano katika nchi hii ya Kusini Mashariki mwa Asia yamekuwa nadra kwa sababu ya vizuizi vilivyokusudiwa kupambana na Covid-19.

Suala la ufisadi hata hivyo ni nyeti sana nchini Malaysia, hasa tangu fuko la utawala, 1MDB, ambalo, mnamo 2018, ilichangia kuanguka kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak, aliyeshtakiwa kwa ufisadi.

Bw. Azam, ambaye alikuwa mkuu wa uchunguzi wakati wa ubadhirifu huu wa dola bilioni kadhaa za mfuko wa utawala 1MDB, zilizopaswa kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Malaysia, amekuwa chini ya uangalizi kwa wiki kadhaa, akishukiwa na shughuli za biasharakwa kuwakilisha mtu mwengine baada ya kukiri kuruhusu ndugu yake kutumia akaunti yake.

Amekana kufanya makosa yoyote, huku mdhibiti wa dhamana wa Malaysia akimuonya wiki hii. Hii, hata hivyo, haikutuliza hasira ya raia.

"Tulikuja kwa sababu hatuwezi kuruhusu ufisadi kuendelea," Mohamad Zawawi Ishak, 29, ameliambia shirika la habari la AFP wakati umati wa watu ulikusanyika nje ya kituo cha gari moshi mjini karibu saa tano mchana saa za Malaysia.

"Katika vita dhidi ya rushwa, fisadi lazima tupambane naye".

Sivaranjani Manickam, 41, amesema serikali inahimiza ufisadi zaidi kwa kutomwadhibu Bw Azam. "Hasira inatufanya tuende barabarani leo kuandamana," ameeleza.

Polisi walifunga njia kuu kadhaa katika mji mkuu na maafisa kadhaa wa sheria walitumwa, wengine wakiwa na vifaa vya kutuliza ghasia, kabla ya umati wa watu kutawanyika chini ya masaa mawili baadaye.

Mjumbe wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa zaidi ya miaka 36, ​​Bw Azam aliteuliwa kuwa mkuu wa taasisi hiyo mwaka 2020, huku kukiwa na jitihada za kurejesha fedha zilizokuwa zimefujwa.

Mwaka huo huo, mkuu wa zamani wa serikali Najib Razak alipatikana na hatia ya rushwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela. Anasubiri rufaa ya mwisho katika mahakama ya juu zaidi ya taifa na anakabiliwa na kesi nyingine mbili zinazoendelea kuhusiana na kashfa ya 1MDB.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.