Pata taarifa kuu
KAZAKHSTAN-USALAMA

Kazakhstan: Rais adai kuwa ghasia zilizozuka ilikuwa ni jaribio la 'mapinduzi'

Utulivu unaonekana kurejea Kazakhstan baada ya karibu watu 8,000 kukamatwa baada ya wiki moja ya ghasia zilizoambatana na ukandamizaji mkubwa. Siku moja ya maombolezo pia ilitangazwa Jumatatu nchini Kazakhstan.

Afisa wa manispaa karibu na eneo kuu huko Almaty, Januari 10, 2022.
Afisa wa manispaa karibu na eneo kuu huko Almaty, Januari 10, 2022. REUTERS - PAVEL MIKHEYEV
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki ya ghasia ambazo zilibadilika na kuwa ghasia zenye machafuko, hasa katika mji wa Almaty, mji mkuu wa kiuchumi wa Kazakhstan, mamlaka imetangaza kwamba wamedhibiti tena hali hiyo. Usafiri wa umma unaanza tena katika jiji kubwa zaidi la Kazakhstan na huduma ya inteneti imerejeshwa baada ya kukatika kwa muda wa siku tano.

Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev pia aliwafuta kazi maafisa wawili wakuu wa usalama siku ya Jumapili, na kuongeza kasi ya kusafisha idara ya usalama ya nchi hiyo.

"Lengo lao kuu lilikuwa bila shaka: kudhoofisha katiba"

Jumatatu hii, Januari 10, alielezea matukio hayo mbele ya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin na washirika wake wengine wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO), akibaini kwamba operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi ilikuwa ikienelea.

"Matukio yote tangu kuanza kwa mwaka huu ni sehemu ya mpango ulioandaliwa kwa muda mrefu," alisema. Wanaharakati wenye silaha waliokuwa wakisubiri walijiunga na maandamano. Lengo lao kuu lilikuwa wazi: kudhoofisha utaratibu wa kikatiba, kubadili taasisi za serikali na kuchukuwa madaraka. Lilikuwa ni jaribio la mapinduzi. "

Aliwahakikishia kuwa vikosi vya Kazakhstan "havijawahi kutumia na kamwe havitatumia nguvu za kijeshi dhidi ya waandamanaji wa amani," aliongeza. Tutakomesha kwa uthabiti aina zote za itikadi kali na vurugu pamoja na vitendo vya kutumia silaha dhidi ya Kazakhstan. Operesheni kubwa inayoendelea ya kukabiliana na ugaidi itakoma hivi karibuni, ni dhamira ya ufanisi na yenye mafanikio ya askari wa CSTO. Jambo muhimu ni kwamba matukio haya hayatafanyika tena. "

Hata hivyo, mamlaka haijachatoa ushahidi wowote wa kuhusika kwa "magaidi" au vikosi vya kigeni.

Wakati ho huo wizara ya mambo ya ndani imebaini kwamba vikosi vya usalama nchini Kazakhstan vimewakamata jumla ya watu 7,939 kufikia leo jumatatu kufuatia machafuko yaliyoenea katika nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.