Pata taarifa kuu
JAPAN

Coronavirus: Tokyo katika tahadhari, hospitali zakabiliwa na shinikizo

Tahadhari ya afya imewekwa leo Alhamisi kwenye kiwango cha juu katika mji mkuu wa Japan, Tokyo, ambapo visa vipya 822 vya maambukizi ya COVID-19 vimegunduliwa kwa muda wa saa 24, ikiwa ni rekodi.

Maofisa wa afya wa Japan katika moja ya ukaguzi wa virusi vya Corona
Maofisa wa afya wa Japan katika moja ya ukaguzi wa virusi vya Corona Philip FONG / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Idara ya huduma za matibabu zimetumia vifaa vyote vilivyokuepo kukabiliana na ugonjwa hatari aw COVID-19, na kwa sasa ghala zko tupu," Masataka Inokuchi, Naibu kiongozi wa chama cha Madaktari jijini Tokyo, amesema katika mkutano wa kamati ya kuzuia na kudhibiti janga hilo mbele ya Gavana wa Tokyo, Yuriko Koike.

 

"Kupunguza idadi ya wagonjwa (wa COVID-19) itakuwa njia pekee ya kutumia", ameongeza

 

Rekodi ya awali ya visa vipya vya kila siku, iliyoripotiwa Jumatano wiki hii , ilikuwa ya vifo vipya 678 vya maambukizi.

 

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019..

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.