Pata taarifa kuu
ARMENIA-AZERBAIJAN-MAREKANI-USALAMA

Nagorno-Karabakh: Marekani yatangaza mkataba mpya wakati vita vikiendelea

Marekani imetangaza mkataba mpya wa kibinadamu ambao utaanza kutekelezwa leo Jumatatu huko Nagorno-Karabakh, wakati mapigano yalizuka tena Jumapili kati ya Azerbaijan na wanaharati waliojitenga wa Armenia.

Kundi la Minsk, lililopewa jukumu na Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) kwa kusuluhisha mzozo huo, imesema wenyeviti wenza na mawaziri wa mambo ya nje walikubaliana kukutana tena huko Geneva mnamo Oktoba 29.
Kundi la Minsk, lililopewa jukumu na Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) kwa kusuluhisha mzozo huo, imesema wenyeviti wenza na mawaziri wa mambo ya nje walikubaliana kukutana tena huko Geneva mnamo Oktoba 29. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Pande hizo mbili zinaolaumiana kwa kuvunja mkataba wa awali wa kusitisha mapigano.

Katika taarifa ya pamoja, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani na serikali ya Azerbaijan na Armenia zimebaini kwamba mkataba wa kusitisha mapigano utaanza kutukelezwa leo Jumatatu asubuhi saa 8:00.

"Hongera kwa Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian na rais wa Azerbaijan Ilham Aliev, ambao wamekubaliana tu juu ya kusitisha mapigano (...) Maisha ya watu wengi yataokolewa," rais wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Tangazo hilo lilitolewa siku mbili baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kufanya mazungumzo na pande tofauti huko Washington na wenzake wa Armenia na Azerbaijan. Marais wenza wa kundi la Minsk (Marekani, Urusi, Ufaransa) pia walishiriki katika mikutano hii.

Wakati wa "mazungumzo", "marais wenza na mawaziri wa mambo ya nje walijadili kuhusu utekelezaji wa haraka wa mkataba wa kibinadamu wa usitishaji vita, vigezo vinavyowezekana vya uthibitisho wake, na walijadiliana kuhusu mambo mujimu ya suluhisho kamili, " walisema katika taarifa ya pamoja.

Kundi la Minsk, lililopewa jukumu na Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) kwa kusuluhisha mzozo huo, limesema wenyeviti wenza na mawaziri wa mambo ya nje walikubaliana kukutana tena huko Geneva mnamo Oktoba 29.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.