Pata taarifa kuu
CHINA-BEIJING-CORONA-AFYA

Coronavirus: Safari za ndege zafutwa kwenye viwanja vya ndege vya Beijing

Mamlaka ya afya nchini China imetangaza visa vipya 31 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika mji wa Beijing kwa siku ya Jumanne pekee, maambukizi yanayohusiana na mlipuko wa pili wa Covid-19 ulioanzia kwenye masoko mawili ya mji huo.

Karibu asilimia 15  ya safari za ndege zimefutwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing.
Karibu asilimia 15 ya safari za ndege zimefutwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi mapya ya virusi katika mji wa Beijing, mamlaka ya mji huo imechukua hatua ya kufuta safari zote za ndege za kuingia na kutoka.

Baada ya miezi miwili kutoripotiwa kisa chchte cha maambukizi, jumla ya watu 137 wamepatikana na virusi vya Corona tangu wiki iliyopita katika mji huo wenye wakazi milioni 21. Mlipuko huo wa pili ulianzia kwenye soko ya chakula ya mji wa Beijing.

Kulingana na taarifa ya manispaa ya jiji, mji mkuu wa China umerekodi leo Jumatano visa vipya 31 vya maambukizi kwa siku peke ya jana Jumanne.

Shule zote zimetakiwa kufungwa katika mji mkuu wa China, katika kukabiliana na kusambaa kwa maambukizi hayo mapya, kwa mujibu wa vyanzo kutoka maispaa ya jiji la Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.