Pata taarifa kuu
JAPANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Tokyo yaondoa hali ya dharura katika sehemu kubwa ya Japani

Serikali ya Japani imetangaza kuondoa hali ya dharura katika sehemu kubwa ya nchi hiyo, mwezi mmoja baada ya kutangazwa katika kupambana na mgogoro wa kiafya unaotokana na Corona.

Waziri Mkuu Shinzo Abe na Waziri wa Afya Katsunobu Kato katika mkutano wa dharura kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, Tokyo Februari 14, 2020.
Waziri Mkuu Shinzo Abe na Waziri wa Afya Katsunobu Kato katika mkutano wa dharura kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, Tokyo Februari 14, 2020. STR / JIJI PRESS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya hatua hiyo mji mkuu Tokyo utaendelea kuwa chini ya vizuizi vilinavyolenga kudhibiti janga la Corona.

Waziri wa Uchumi Yasutoshi Nishimura amesema pendekezo la serikali la kuondoa hali ya dharura katika mikoa 39 kati ya 47 ya Japani limekubaliwa na jopo la wataalam.

Kwa pamoja, wilaya 39 zina 54% ya wakazi wa nchi hiyo.

Kesi 16,103 za maambukizi ya virusi vya Corona zimethibitishwa nchini Japani, pamoja na vifo 696, huku wagonjwa 9,868 wamepona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.