Pata taarifa kuu
URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu visa 100,000 vya maambukizi vyathibitishwa Urusi

Urusi imetangaza visa vipya 5,841 vya maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya masaa 24, na kufikisha idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa kufikia 99,399.

Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.
Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya. REUTERS/Alexey Nasyrov
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na vifi vipya108 vilivyotokana na COVID-19 ndani ya masaa 24 yaliyopita, idadi ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo sasa imefikia 972, kulingana na mamlaka ya afya nchini Urusi.

Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.

"Tunaona kuwa hali inabadilika kila siku na kwa bahati mbaya inazidi kuwa mbaya. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka, haswa idadi ya wale walio na hali mbaya inazidi" alisema.

Putin, ambaye hivi karibuni alifanya tathmini juu ya ugonjwa wa Covid-19 katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video, alisema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.

Rais Vladimir Putin alibaini kuwa, ikiwezekana, vifaa vya jeshi pia vinaweza kutumiwa kupambana na janga hilo, ambalo Umoja wa Mataifa ulisema linatishia ulimwengu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.