Pata taarifa kuu
URUSI-CORONA-AFYA

Daktari aliyekutana na Putin wiki iliyopita apatikana na virusi vya Corona

Daktari aliyekutana na rais wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita alipokuwa akizuru hospitali moja huko Moscow, amepatikana na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo, Televisheni ya serikali, Rossiya 24, imeripoti leo Jumanne.

Daktari Denis Protsenko aliyekutana na Putin wiki iliyopita apatikana na virusi vya Corona.
Daktari Denis Protsenko aliyekutana na Putin wiki iliyopita apatikana na virusi vya Corona. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi alizuru hospitali ya Kommunarka Jumanne wiki iliyopita ambapo alikutana na daktari mkuu wa hospitali hiyo Denis Protsenko. Wote wawili hawakuwa wamevaa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa mazungumzo yao.

"Hali ni shwari," ofisi ya rais wa Urusi (Kremlin) imesema, ikinukuliwa na shirika la habari la RIA, huku ikikumbusha kwamba Vladimir Putin huwa anafanyiwa vipimo mara kwa mara.

Hadi leo, janga la Corona, ambalo lilianzia nchini China mwezi Desemba kabla ya kuenea duniani kote, limesababisha vifo vya watu 17, na watu 2,337 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, kulingana na ripoti rasmi iliyotolewa na mamlaka nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.