Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Watu waliotekeleza shambulio Istanbul wajulikana

Viongozi wa Uturuki wamewatambua Alhamisi hii watu watatu wa kujitoa mhanga katika mashambulizi matatu yaliyotokea Jumanne jioni wiki hii katika uwanja wa ndege wa Istanbul, mashambulizi ambayo yalisababisha vifo vya watu 43, ikiwa ni pamoja na raia 19 wakigeni.

Vikosi vya usalama vya Uturuki vikipiga doria katika uwanja wa ndege wa Istanbul, tarehe 30 Juni 2016.
Vikosi vya usalama vya Uturuki vikipiga doria katika uwanja wa ndege wa Istanbul, tarehe 30 Juni 2016. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Magaidi hao kwa mujibu wa serikali ya Uturuki ni kutoka nchi ya Urusi, Uzbekistan na Kyrgyzistan. Hata hivyo hakuna kundi hata moja lililodai kutekeleza shambulio hilo, lakini kundi la Islamic Statelilinyooshewa kidole kuhusika katika shambulio hilo na polisi ya Uturuki iliwakama watu 13.

Uraia wa watuhumiwa hao 13 waliokamatwa Alhamisi hii haujajulikana wala mashtaka ambayo yanaweza kufunguliwa dhidi yao. Polisi iliendesha operesheni hiyo katika maeneo kumi na sita tofauti katika mji wa Istanbul, misako mingine ilifanyika katika mji wa Izmir.

Kwa mujibu wa serikali ya Uturuki, watu 3 ndio waliendedha mashambulizi matatu katika uwanja wa ndege. Watu hao ni kutoka nchi ya Urusi, Uzbekistan na Kygyzistan, huu wa mwisho ni mwenye asili ya Jamhuri ya Dagestan au Chechnya.

Uchunguzi unaendelea na mazingira ya shambulio hilo yanaeleweka. Serikali ya Uturuki inataka uchunguzi huo kufanyika haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.