Pata taarifa kuu
YEMEN-Usalama

Yemen yakabiliwa na mdororo wa usalama

Serikali ya Marekani imesema haitakubali kujihusisha na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Yemen dhidi ya makundi ya kiisilamu yanayotuhumiwa kuhusika na mashambulizi nchini humo.

Mmoja kati ya majeruhi aondolewa katika eneo la tukio katika mji wa Sanaa, nchini Yemen, Oktoba 9 mwaka 2014.
Mmoja kati ya majeruhi aondolewa katika eneo la tukio katika mji wa Sanaa, nchini Yemen, Oktoba 9 mwaka 2014. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri baada ya kuwepo kwa taarifa za watu kadhaa kujeruhiwa katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya mabomu matano kulipuka kando ya barabara.

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Yemen, mabomu hayo yalikuwa yakiwalenga wapiganaji wa Houthi wa madhehebu ya Shia.

Maafisa wa usalama walifanikiwa kutegua mabomu mengine mawili. Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na mashambulizi hayo.

Vuguvugu la Houthi Ansarullah lenye mafungamano na Washia kutoka Iran limekuwa nguvu kuu ya kisiasa nchini Yemen baada ya kuuteka mji mkuu Sanaa mwezi Septemba.

Wakati huohuo askari polisi aliuawa Yemen katika shambulizi linalodaiwa kuwa la kigaidi.

Shambulio hilo lilitokea Jumatatu desemba 8 jioni katika eneo la Damistan, kijiji kinachokaliwa na jamii ya Washia kusini magharibi mwa mji wa Manana, ambapo askari polisi alikua akiendesha shughuli yake, wizara ya mambo ya ndani imeeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.