Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

Hong Kong: waandamanaji waendelea kuishinikiza serikali

Hali ya utulivu imeendelea kuripotiwa katika mji wa Hong Kong, huku maeneo matatu yakiendelea kukaliwa na waandamanaji wanaodai mageuzi kwenye uchaguzi wakibaini kwamba hauendani na mfumo wa kidemokrasia.

Waandamanaji waendelea na msimamo wao katika eneo la kibiashara la Mongkok (Hong Kong).
Waandamanaji waendelea na msimamo wao katika eneo la kibiashara la Mongkok (Hong Kong). REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano takribani wandamanji 300 wamelala kwenye barabara za miji ya Admiratly, Causeway Bay na Mangkok

Bunge la jimbo la Hong Kong, limeamua kuahirisha kikao chake kiliyokua kimepangwa kufanyika leo Jumatano kutokana na hali inayo jiri katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo. Ni kwa mara ya kwanza Bunge la jimbo la Hong Kong linaahirisha kikao chake kufuatia maandamano tangu Hong Kong ijiunge na China mwaka 1997.

Kwa ombi la wabunge 41 wanaounga mkono utawala wa Pekin, milango ya jengo la Bunge itaendelea kufungwa. Kwa mujibu wa wabunge hao, ni vigumu wabunge kuendelea kushiriki vikao vya Bunge wakati baadhi ya majengo ya serikali bado yanakaliwa na waandamanaji.

Wabunge wanaounga mkono uwepo wa mfumo wa kidemokrasia wamepinga uamzi huo wakibaini kwamba ni mbinu za kutaka kuendelea kuchochea mvutano kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu na wakaazi wa Hong Kong.

Wabunge wanaounga mkono mfumo wa kidemokrasia wamependekeza kuwepo na mjadala kuhusu namana ya kutafutia suluhu maandamano hayo na kuepusha makabiliano ya mara kwa mara kati ya waandamanaji na polisi.

Mada hiyo ndiyo itagubika mkutano wa kwanza wa wanafunzi wa vyuo vikuu na afisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Hong Kong, Carrie Lam, utakaoanza Ijumaa wiki hii. Waandamanaji hao wanaokalia miji maeneo matatu muhimu ya mji wa Hong Kong wameapa kuendelea kuishinikiza serikali ili itekeleze madai yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.