Pata taarifa kuu
UFILIPINO

Kimbunga Haiyan chapiga Ufilipino na kusababisha vifo vya watu 3

Kimbunga kujilikanacho kwa jina la Super Typhoon Haiyan kimeanza kupiga nchini Ufilipino leo ijumaa na kusababisha vifo vya watu watatu. Kimbunga hicho kilichoambatana na upepo mkali uanaovuma kwa kasi ya takribani kilometa 315 kinatajwa huenda kikawa kibaya zaidi kulikumba Taifa hilo na kimesababisha maelfu ya watu kuhamishwa kutoka katika makazi yao.

NOAA/AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Serikali imethibitisha idadi ya vifo hivyo na kusema huenda ikaongezeka kutokana na watabiri wa hali ya hewa kusema huenda madhara zaidi iwapo hali mbaya ya hewa itaendelea kushuhudiwa.

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema limepokea ripoti za uharibifu mkubwa wa majengo, kuanguka kwa miti na uharibifu wa miundombinu.

Kimbunga hicho kimesababisha kukatika kwa huduma za mawasiliano ya simu, kusitishwa kwa usafiri wa ndege na majini, na shule zimefungwa ili kuepuka madhara zaidi.

Kisiwa cha Bohol ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho na pia kiliathiriwa na tetemeko la ardhi la mwezi uliopita ambalo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 220.

Waathirika wa tetemeko la mwezi uliopita zaidi ya 5000 bado wamehifadhiwa katika mahema na we

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.