Pata taarifa kuu
CHINA-MAHAKAMA

Kiongozi wa zamani wa chama cha kikominist nchini China Bo Xilai apandishwa kizimbani

Aliyekuwa kiongozi wa juu wa chama cha kikomunist nchini China na mwanasiasa mwenye nguvu, Bo Xilai hii leo amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya mjini Jinan kujibu mashtaka ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi yanayomkabili.

Mahakama nchini China ikionyesha picha ya Bo Xilai
Mahakama nchini China ikionyesha picha ya Bo Xilai
Matangazo ya kibiashara

Jaji anayesikiliza kesi hiyo alitangaza kuanza rasmi kwa kesi dhidi ya kiongozi huyo na kumtaka kuwepo mahakamani wakati mwendesha mashtaka wa serikali akimsomea mashtaka yanayomkabili.

Bo Xilai anakabiliwa na kesi dhidi ya kupokea hongo ili kutoa zabuni kwa makampuni makubwa nchini humo, ubadhilifu wa mali na kutumia madaraka yake vibaya.

Iwapo atapatikana na hatia kiongozi huyo anakabiliwa na adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria za China.

Mahakama hiyo ya China imeonyesha picha ya kiongozi huyo wa zamani anaye kabila na mashataka ya rushwa  Bo Xilai akisimama kizimbani ikiwa ni mara ya kwnza kuonekana kwa kipindi cha miezi 17.

Picha hiyo inamuonyesha kiongozi huyo akisimama na maafisa wawili wa polisi, ambao wamevaa shati nyeupe na suruali nyeusi, na amekuwa kizuizini tangu machi mwaka 2012 katika eneo lisilo julikana.

 Bo, mwenye umri wa miaka 64, alijikuta katika sakata la kashfa kubwa la rushwa lililokikumba chama cha Kikomunisti kwa miongo kadhaa.

Kiongozi huyo anakabiliwa na adhabu ya kifo iwapo atadhihirika kuhusika. Kesi hiyo inafanyika katika Mahakama ya Jinan, ILIPO katika jimbo la mashariki la Shandong.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.