Pata taarifa kuu
Afghanistani

Wapiganaji wa Taliban wasifu hatua ya kufunguliwa Ofisi nchini Qatar

Wapiganaji wa Taliban wamesifu hatua ya kufunguliwa kwa Ofisi nchini Qatar wakisema kuwa hiyo inaashiria mafanikio na kuapa kupambana mpaka pale Majeshi yote ya Marekani yatakapoondoka nchini Afghanistani.

Wawakilishi wa Ujumbe wa Taliban wakiwa katika shughuli za kufungua Ofisi yao nchini Qatar
Wawakilishi wa Ujumbe wa Taliban wakiwa katika shughuli za kufungua Ofisi yao nchini Qatar Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kufunguliwa kwa Ofisi nchini Qatar kumeonekana kuwa hatua ya kwanza kuelekea Makubaliano ya amani wakati ambapo Majeshi ya NATO yanapokamilisha kazi yake mwishoni mwa mwaka ujao, halikadhalika Serikali ya Kabul imeshutumu upinzani kujitengenezea sura ya kuwa Serikali uhamishoni.
 

Wapiganaji wa Taliban wamekaribisha kwa mikono miwili hatua ya kufunguliwa kwa Ofisi nchini Qatar na kusema kuwa sasa wataweza kufaya mazungumzo na jumuia ya kimataifa wakiwa kama Taifa huru.
 

Katika hatua nyingine,Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameendelea kutia ngumu kwa serikali yake kushiriki kwenye mazungumzo ya moja kwa moja ya pande tatu ambayo yatalishirikisha Kundi la Wanamgambo wa Taliban na Serikali ya Marekani.

Serikali ya Kabul imekataa kushiriki kwenye mazungumzo hayo yaliyoitishwa na Marekani ikitaka Ofisi ya Kundi la Taliban iliyofunguliwa nchini Qatar ibadilishwe jina na isitambulike kama Ubalozi.

Serikali ya Marekani imejitokeza kwa mara nyingine na kutangaza kuahirisha mazungumzo hayo ambayo yalipangwakufanyika hivi karibuni hadi utata uliopo utakaposuluhishwa kama anavyoeleza Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Jennifer Rene Psaki.

Awali Serikali ya Afghanistan ilikuwa tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo na mahasimu wao wa Taliban kusaka suluhu ya mgogoro wao lakini walitibuliwa nyongo na kufunguliwa kwa Ofisi ya Kundi hilo huko Qatar na kupewa jina la Ubalozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.