Pata taarifa kuu
Afghanistani

Majeshi ya NATO yakabidhi jukumu la ulinzi na usalama kwa Vikosi vya Afghanistani

Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai ametangaza hatua ya Majeshi ya kujihami ya NATO, kukabidhi jukumu la kulinda usalama nchi nzima mikononi mwa Vikosi vya Afghanistani akisema kuwa kuanzia hapo kesho Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Afghanistani watakua wakiongoza jitihada za kulinda usalama.

Rais wa Afghanistani Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani Hamid Karzai REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Majeshi ya NATO Anders Fogh Rasmussen amesema kuwa Vikosi vya Afghanistani wataongoza jukumu la kulinda usalama kuanzia siku ya jumanne na kuwataka Raia wa nchi hiyo kuwaunga mkono.
 

Sherehe za kukabidhi Miji 95 kutoka katika udhibiti wa NATO kwenda kwa Afghanistani unahusisha maeneo ya kusini na Mashariki mwa nchi hiyo, ambapo Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya Serikali tangu mwaka 2001.
 

Baada ya ya kukabidhiana mamlaka ya ulinzi na usalama, wanajeshi 100,000 wa NATO watakuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa Wanajeshi na Askari wa nchini humo ili kuwawezesha kuongoza mapambano dhidi ya Wanamgambo wa Taliban.
 

Hata hivyo kumekuwepo na shuku juu ya uwezo wa Wanajeshi 350,000 kupambana na Wanamgambo wa Taliban wakati huu ambapo majeshi ya NATO watashughulikia maswala mengine yahusuyo vifaa kama itahitajika.
 

Mashambulizi ya hivi karibuni yanadhihirisha uwezo wa Taliban kushambulia mji wa Kabul wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi wa Urais na kuondoka kwa Vikosi vya NATO mwishoni mwa mwaka 2014.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.