Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Ulinzi waimarishwa nchini Bangladesh huku maandamano ya siku mbili yaliyoitishwa na Upinzani yakianza

Jeshi la Polisi nchini Bangladesh limeimarisha ulinzi mkali katika Mji Mkuu Dhaka ikiwa ni tahadhari ya kukaa tayari kukabiliana na ghasia zozote zinazoweza kuzuka wakati maandamano yaliyoitishwa na Vyama vya Upinzani yakiendelea kupinga mauaji ya waumini wa Kiislam yaliyofanywa mwanzo mwa juma. Maelfu ya Polisi wamesambazwa katika mitaa ya Jiji la Dhaka wakiwa wamejihami barabara kwa mabomu ya machozi na risasi za mpira kukabiliana na upinzani wowote ambao unaweza ukatolewa na waandamanaji ambao wamechukizwa na hivyo vya waumini hao wa Kiislam.

Polisi nchini Bangladesh wakiwa wameshika doria katika Jiji la Dhaka kukabiliana na waandamanaji watakaosababisha ghasia
Polisi nchini Bangladesh wakiwa wameshika doria katika Jiji la Dhaka kukabiliana na waandamanaji watakaosababisha ghasia
Matangazo ya kibiashara

Shughuli nyingi zimesimama kwenye Jiji la Dhaka huku biashara, mashule na ofisi vyote vikifungwa kutokana na kuhofia kutokea kwa ghasia zinazoweza zikasababisha umwagali wa damu na hata uharibifu wa mali mbalimbali.

Mkuu wa Polisi katika Jiji la Dhaka Mohammad Moniruzzaman amesema wapo tayari kukabiliana na uvunjifu wa amani wowote ambao unaweza ukafanywa na waandamanaji hao ambao wanataka hatua sitahiki zichukuliwe dhidi ya waliofanya mauaji ya waumini hao.

Chama Kikuu Cha Upinzani nchini Bangladesh cha BNP kwa kushirikiana na Shirika la Kiislam la Hefajat-e-Islam ndiyo wameistisha maandamano hayo ya siku mbili kuanzia leo na kuendelea hadi kesho kupinga mauaji yaliyofanywa dhidi ya waumini wa Kiislam walioandamana kushinikiza uwepo wa hatua kali ya kukufuru.

Jumla ya waumini wa Dini ya Kiislam wapatao 38 wamepoteza maisha kwenye mapambano makali yaliyozuka jioni ya jumapili kati yao na Jeshi la Polisi lililotumia nguvu kubwa kuwasambaratisha katika mitaa ya Jiji la Dhaka.

Waratibu wa Maandamano hayo ya siku mbili wamesema wanataka kufikisha ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa ili iweze kuona ni kwa namna gani serikali imekuwa aiheshimu haki za binadamu katika taifa hilo.

Jumuiya ya Kiislam ya Hefajat-e-Islam inayotajwa kuchcochea kutokea kwa maandamano ya awali imesema itaendelea kupambana kuhakikisha kilio chao kinapata jibu na sheria hiyo ya kukufuru inaongezewa makali ili atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa hilo anyongwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.