Pata taarifa kuu
Syria

Watu 8 wauawa na vikosi vya Syria

Takriban watu wanane wameuawa na vikosi vya usalama nchini Syria hapo jana wakati wa msako mkali dhidi ya waandamanaji wanaompinga rais wa nchi hiyo,bashar Al Assad ikiwa ni miezi sita tangu kuanza kwa maandamano hayo nchini Syria.

Reuters/Handout
Matangazo ya kibiashara

Ingawa waandamanaji wamekuwa wakidhibitiwa na vikosi vya serikali,waandamanaji wamepanga kuwa na maandamano makubwa hii leo kuadhimisha miezi sita ya maandamano tangu tar 15 mwezi march waandamanaji walipoingia miataani kwa mara ya kwanza kudai mabadiliko.

Hapo jana wanajeshi na vikosi vya usalama vilivamia vijiji na maeneo ambapo waandamanaji walikisiwa kuwepo,waangalizi wa maswala ya haki za binaadam nchini Syria wamethibitisha.

Kwa mujibu wa kundi hilo vikosi vilivamia vikiwa na silaha na kuweka vituo vya upekuzi kisha vilikamata raia 100.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.