Pata taarifa kuu
Japan

Maafisa watatu watimuliwa kutokana na uvujaji wa nyuklia Japan

Maafisa wa watatu waliokuwa wakishughulikia usalama na sera za nishati ya nyuklia wametimuliwa kazi kutokana na tatizo linaloendelea la kuvuja kwa vinu vya nyuklia vya Fukushima Daiichi hali iliyosababishwa na Tsunami.

Reuters/Tokyo Electric Power Co
Matangazo ya kibiashara

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Banri Kaieda amesema kuwa maafisa watatu wa ngazi za juu wanapaswa kuwajibika kutokana na kile kinachotokea nchini Japan.

Tatizo hilo bado linaendelea tangu kuanza kwake kipindi cha miezi mitano na mionzi ya nyuklia imekuwa ikiendelea kuvuja hali inayoashiria kuwa maafisa hao wameshindwa kutekeleza wajibu.

Maafisa waliotimuliwa ni pamoja na mkuu wa wakala wa usalama wa nyuklia Nobuaki Terasaka, mkuu wa wakala wa rasilamli na nishati, Tetsuhiro Hosono na naibu waziri wa uchumi, biashara na viwanda Kazuo Matsunaga.

Hata hivyo waziri Kaieda ambaye alitangaza kutimuliwa kwa maafisa hao ambaye pia ameshiriki kwa kiasi kikubwa kushughulikia tatizo hilo amesema hata yeye mwenyewe anafikiria kujiuzulu kama njia ya kuwajibika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.