Pata taarifa kuu
Bahreini

Chama kikuu cha upinzani nchini Bahreini cha tishio kujiondowa katika mazungumzo na serikali

Chama kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha the Islamic Accord Association kimetishia kujiondoa katika mazungumzo na serikali endapo utawala wa kifalme wa nchi hiyo utashindwa kufanya mabadiliko wanayoyahitaji.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo kati ya serikali, vyama vya upinzani, na wanaharakati yalianza juma moja lililopita ambapo zaidi ya taasisi na vyama zaidi ya 60 vilishiriki mazungumzo hayo ambayo yanalenga kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa nchini humo.

Khalil al-Marzooq kiongozi wa chama hicho cha upinzani amesema kuwa wao watapinga mazungumzo kuhusu mambo ya uchumi na kijamii lakini wataendelea kushiriki katika vikao vitakavyozungumzia hali ya siasa nchini humo.

Chama hicho kimesema kuwa kinaamini lengo la mazungumzo hayo ni kujadili hali ya kisiasa na usalama wa taifa hilo na sio vinginevyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.