Pata taarifa kuu
PHILIPPINE

Serikali ya Philippine yaanza mazungumzo na viongozi wa kundi la kiislamu la MIFL

Viongozi wa serikali ya Philippine wameanza mazungumzo na viongozi wa kundi la Kiislamu lenye msimamo mkali nchini humo la Moro Islamic Liberation Force ambalo limekuwa likifanya uasi kusini mwa nchi hiyo.

Ramani kuonyesha mji wa Mindanao nchini Philippine
Ramani kuonyesha mji wa Mindanao nchini Philippine Diplomatie.gouv.fr
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ambayo yanafanyika mjini Kuala Limpur nchini Malaysia yanalenga kumaliza mgogoro wa muda mrefu uliokuwepo nchini humo baina ya kundi hilo na vikosi vya serikali.

Kundi hilo la MIFL lilianza uasi kusini mwa nchi ya Philippine katika jimbo la Mindanao mnamo mwaka 1978 ambapo watu zaidi laki moja na elfu hamsini waliuawa tangu kuanza kwa machafuko hayo ambapo kundi hilo limekuwa likishinikiza eneo hilo kuwa la waislamu.

Mazungumzo haya yanakuwa ni ya pili kufanyika kufuatia yale ya mwaka 2003 kuvunjika baada ya pande hizo mbili kushindwa kutekeleza kile ambacho walikubalina mjini Manila.

Mapema mwezi wa nne mwaka huu kundi hilo lilipeleka mapendekezo ambayo wameitaka serikali kuja na majibu yake wakati wa mkutano huu ambao umeanza hii leo mjini Manila kabla ya kuendelea mbele zaidi kwa mazungumzo.

Mmoja wa maofisa wa serikali anayeshiriki mazungumzo hayo amesema kuwa kwa upande wao pia wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwa kundi hilo yanayolenga kuwataka kuweka silaha chini kabla ya kuendelea na mazungumzo.

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati ambapo kundi hilo la kiislamu limekuwa likifanya mashambulizi ya kujitoa muhanga katika jimbo la Mindanao na mji wa Manila kushinikiza serikali kutekeleza matakwa yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.