Pata taarifa kuu
Iran-Teheran

Mwanasiasa aachiwa huru nchini Iran

Serikali ya Iran imemuachia huru Mtetezi wa Haki za Binadamu Emadeddin Baghi baada ya kumshikilia kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa tuhuma za kusambaza propaganda dhidi ya utawala wa nchi hiyo.

Mpinzani aliachiwa huru nchini Iran
Mpinzani aliachiwa huru nchini Iran Iranvox
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria wa Baghi, Saleh Nikbakht amethibitisha kuachiwa kwa mteja wake ambaye alikumbana na adhabu ya kifungo cha miaka mitano kutojihusisha na siasa kutokana na kueneza propaganda.

Baghi mwenye umri wa miaka arobaini na kenda amekuwa ni miongoni mwa waandishi wa habari na mtetezi wa Haki za Binadamu ambaye amekuwa mkosoaji mkali dhidi ya Utawala wa Rais Mahmoud Ahmadinejad.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.