Indonesia
Kesi ya kiongozi wa kidini nchini Indonesia Abu Bakar Bashir yasikilizwa chini ya ulinzi mkali
Usalama umeimarishwa nchini Indonesia huku mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu tuhuma za ugaidi zinazomkabili kiongoni wa dini ya kiislamu Abu Bakar BashirMaafisa wa usalama wanasema kuwa zaidi ya askari elfu tatu wamepiga kambi katika jiji la Jakarta pamoja na maeneo yanayokaribia mahakama hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Bashir mwenye umri wa miaka 72, anatuhumiwa kupanga na kufadhili mafunzo ya Jihad magharibi mwa nchi hiyo, shutuma ambazo amekuwa akipinga kwa kusema kuwa ni swala halali kulingana na dini ya kiiislamu.
Ikiwa kiongozi huyo atapatiakana na makosa, atafungwa kifungo cha maisha jela.