Pata taarifa kuu

Marekani: Rais Biden anataka kupunguza uwekezaji katika teknolojia nchini China

Rais wa Marekani Joe Biden ametia saini agizo la utendaji linalozuia uwekezaji wa teknolojia nchini China na nchi nyingine, Ikulu ya Marekani imetangaza. Hili limezua maandamano "makubwa" kutoka Beijing.

Uamuzi huu, uliochukuliwa kwa jina la ulinzi wa "usalama wa kitaifa" wa Marekani, unajibu hofu ya utawala wa Biden (picha yetu) kwamba China itanufaika na uwekezaji wa Marekani.
Uamuzi huu, uliochukuliwa kwa jina la ulinzi wa "usalama wa kitaifa" wa Marekani, unajibu hofu ya utawala wa Biden (picha yetu) kwamba China itanufaika na uwekezaji wa Marekani. REUTERS - JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

Agizo la kuzuia uwekezaji katika teknolojia linasema kuwa makampuni ya Marekani hayataweza tena kuwekeza kwa uhuru nje ya nchi katika mifumo ya juu zaidi, kama vile akili bandia (AI) au kompyuta, ikiwa inahusu "nchi zenye matatizo", hasa China, imetangaza wizara ya Fedha. Uamuzi huu, uliochukuliwa kwa jina la ulinzi wa "usalama wa taifa" wa Marekani, unajibu hofu ya utawala wa Biden kwamba China itanufaika na uwekezaji wa Marekani katika suala la uhamisho wa teknolojia lakini pia kupitia msaada katika uanzishaji wa mistari ya uzalishaji, kubadilishanamaarifa na upatikanaji wa masoko.

China 'yaghadhabishwa'

Beijing imejibu haraka, kwa kuiandikia Washington siku ya Alhamisi, Agosti 10, kupitia njia za kidiplomasia kwamba inapinga hatua hiyo. "China haijafurahishwa sana na inapinga vikali msisitizo wa Marekani wa kuweka vikwazo kwa uwekezaji nchini China," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema katika taarifa yake, na kuongeza kuwa nchi yake "ina wasiwasi sana na hali hii na inahifadhi haki ya kuchukua hatua." ".

Katika taarifa tofauti, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China ameongeza kusema kuwa agizo hilo "linaachana kabisa na kanuni za uchumi wa soko na ushindani wa haki ambazo Marekani imekuwa ikiukuza kila mara, na huathiri maamuzi ya kawaida ya biashara, inadhuru utaratibu wa biashara wa kimataifa na inavuruga pakubwa usalama wa mitandao ya kimataifa ya viwanda na ugavi”.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.