Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Kuelekea jaribio jipya la nyuklia la Korea Kaskazini, Marekani yasema 'haitashangaa'

Marekani 'haitashangaa' iwapo Korea Kaskazini itafanya jaribio jipya la nyuklia, baada ya jaribio lake la kombora la masafa marefu wiki iliyopita, amesema mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani, Jake Sullivan.

Umoja wa Mataifa, Marekani na washirika wake, ikiwemo Ufaransa, wamelaani vikali urushaji wa kombora hilo, kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa, Marekani na washirika wake, ikiwemo Ufaransa, wamelaani vikali urushaji wa kombora hilo, kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. © Anthony WALLACE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nimekuwa na wasiwasi kwa muda kwamba Korea Kaskazini itafanya jaribio lake la saba la nyuklia," Jake Sullivan amesema katika mahojiano yaliyorushwa siku ya Jumapili kwenye televisheni ya CBS.

"Sioni dalili zozote kwamba hili litatokea hivi karibuni," ameongeza.

"Lakini haitakuwa jambo la kushangaza ikiwa Korea Kaskazini itafanya jaribio jingine la nyuklia kuhusiana na uwezo wake wa makombora ya masafa marefu," ameongeza. Amebaini kwamba Pyonygang ilianza kujaribu uwezo huu miaka kadhaa iliyopita na "inaendelea kufanya hivyo".

Lawama za Umoja wa Mataifa

Siku ya Alhamisi Korea Kaskazini ilisema kwamba imefanikiwa kufanyia majaribio kombora lake jipya la balestiki linalotumia mafuta-imara (ICBM) chini ya usimamizi wa kiongozi wake Kim Jong Un mwenyewe.

Kombora hilo, Hwasong-18 linaloaminika kutumika mara moja tu hapo awali, mnamo mwezi Aprili, lilisafiri kilomita 1,001 katika urefu wa juu wa kilomita 6,648 kabla ya kuanguka katika Bahari ya Mashariki, limesema shirika la habari la serikali la KCNA, likitumia jina la Kikorea la Bahar ya Japan.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alielezea mwaka jana kama "isiyoweza kutenduliwa" hadhi ya nguvu ya nyuklia ya nchi yake na kutoa wito wa kuongezwa kwa utengenezaji wa silaha, hasa silaha za kimkakati za nyuklia.

Umoja wa Mataifa, Marekani na washirika wake, ikiwemo Ufaransa, wamelaani vikali urushaji wa kombora hilo, kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jake Sullivan hata hivyo amesisitiza pendekezo la Marekani la mazungumzo, akihakikisha kwamba Washington iko "tayari kuketi na kujadili mpango wake wa nyuklia bila masharti".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.