Pata taarifa kuu

Colombia: Serikali yazindua upya mazungumzo na waasi wa ELN

Serikali ya Colombia na waasi wa ELN wanaanza tena mazungumzo yao ya amani baada ya kusimama kwa miaka minne. Wawakilishi wao watakutana kuanzia Jumatatu, Novemba 21 alasiri huko Caracas, Venezuela, nchi ambayo ni mpatanishi.

Rais wa Colombia Gustavo Petro akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya Bogota, Agosti 24, 2022.
Rais wa Colombia Gustavo Petro akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya Bogota, Agosti 24, 2022. AP - Fernando Vergara
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo na wapiganaji wa mwisho bado yanaendelea nchini Colombia yalikuwa yamesitishwa chini ya utawala wa Ivan Duque. Mrithi wake, Gustavo Petro, alifanya "amani kamili" na makundi yenye silaha moja ya vipaumbele vya serikali yake.

Orodha kamili ya wajumbe hao ambao watasafiri kuelekea Caracas bado haijafichuliwa na Rais Gustavo Petro. Lakini tayari jina moja linaamsha hisia nyingi. Jina hilo ni la José Félix Lafaurie, mkuu wa wafugaji wa ng'ombe.

'Hatua ya ujasiri'

Mtu ambaye bado anapinga kwa kiasi kikubwa sera yake, kama anvyokumbusha Juan Camilo Restrepo, mpatanishi wa zamani: "Inaonekana kama hatua ya ujasiri ya Gustavo Petro ambayo, kwa njia fulani, inaangamiza sauti za upinzani katika mrengo wa kulia nchini Colombia, kuhusu mazungumzo haya. Hali inaweza kuwa mbaya, kwa sababu hakuna hakikisho kwamba kundi la waasi la ELN litakaribisha uwepo kwenye meza ya mazungumzo wa mtu aliye na historia kama hiyo”.

Mbinu ya kimataifa

Kwa sababu, kama sekta ya ufugaji ni mojawapo ya zilizoathirika zaidi na ghasia za wapiganaji wa msituni, pia imeshiriki kwa kiasi kikubwa katika kufadhili wanamgambo wa mrengo mkali wa kulia ambao wanapambana nao. Makundi yenye silaha yamemwaga damu Colombia kwa zaidi ya nusu karne. Gustavo Petro anataka kuamini katika mtazamo wa kimataifa. Sambamba na ELN, rais wa Colombia anakusudia kufungua mazungumzo na kundi lingine lililojitenga la wa waasi wa FARC na magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.