Pata taarifa kuu

Rais wa Colombia aishtumu Washington kuharibu 'uchumi wote wa dunia'

Rais wa Colombia Gustavo Petro ameishtumu Marekani kwamba inaharibu "uchumi wote duniani". Ameyasema hayo leo Alhamisi, huko Turbo kaskazini-mashariki, akilenga hasa Hifadhi ya Shirikisho la Marekani, FED, ambayo imepandisha viwango vyake muhimu mara tano. Pesa inazidi kuwa ghali, hasa kwa nchi zenye utajiri mdogo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Colombia Gustavo Petro, mjini Bogota, Oktoba 3, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Colombia Gustavo Petro, mjini Bogota, Oktoba 3, 2022. AP - Luisa Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Rais wa kwanza wa mrengo wa kushoto wa Colombia amebaini kwamba mdororo wa kiuchumi unatisha. Mnamo mwezi Machi 2020, viwango vya FED, Hifadhi ya Shirikisho la Marekani, vilikuwa kati ya 0 na 0.25%. Sasa viko kwa 3% au 3.25%.

Gustavo Petro anaamini kwamba viwango hivi vya juu sana vinavutia mtaji kutoka nchi za Amerika Kusini.

Marekani hufanya maamuzi ya kujilinda, wakati mwingine bila kufikiria hatua zake zitahusisha nini. Uchumi wa mataifa ya Amerika Kusini unadhoofika.

"Fedha zetu zote zinashuka, sio tu peso ya Colombia," rais wa Colombia ameongeza.

Hii ni mara ya kwanza ukosoaji wa moja kwa moja unatoklewa kwa Marekani kuhusu suala hili. Balozi wa Marekani nchini Colombia, Francisco Palmieri, amesema.

Sidhani kama tunapaswa kufikiria ni wapi tunapaswa kuweka lawama. Tunapaswa kuzingatia jinsi tunavyoweza, kwa kufanya kazi pamoja, kuimarisha na kukuza maendeleo muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

Kwa wakati huu, peso inaendelea kushuka, na deni la Colombia kwa dola linaweza kuongezeka kwa kupanda kwa viwango vya riba. Sarafu ya Colombia imeshuka thamani kwa 16% dhidi ya dola tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Dola moja sasa ina thamani ya peso 4,700, hali ambayo haijawahi kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.