Pata taarifa kuu

Colombia: Zaidi ya watetezi 120 wa haki za binadamu waliuawa mwaka wa 2022

Idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya 30% ikilinganishwa na mwaka 2021. Rais Gustavo Petro ambaye aliingia madarakani Agosti 7 aliahidi amani kamili. Lakini vurugu hazitoi nafasi. Jumamosi jioni, wakuu wapya wa majeshi, nchi kavu, anga na wanamaji, waliapishwa mbele ya rais wa kwanza wa mrengo wa kushoto katika historia ya nchi hiyo, aliyechaguliwa mwezi wa Juni.

Rais wa Colombia Gustavo Petro (katikati) akiwa amezungukwa na wakuu wapya wa jeshi na Waziri wa Ulinzi Ivan Velasquez (kulia kwake) wakati wa sherehe rasmi Agosti 20, 2022 huko Bogota.
Rais wa Colombia Gustavo Petro (katikati) akiwa amezungukwa na wakuu wapya wa jeshi na Waziri wa Ulinzi Ivan Velasquez (kulia kwake) wakati wa sherehe rasmi Agosti 20, 2022 huko Bogota. REUTERS - LUISA GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

Carlos Rincon alikuwa yule anayeitwa hapa kiongozi wa kijamii, anaeleza mwanahabari wetu huko Bogota, Marie-Eve Detoeuf. Aliishi Puerto Wilches, bandari ndogo ya mto kilomita 400 kaskazini mwa mji wa Bogota. Viongozi walijua kwamba Carlos Rincon alitishwa sana. Idara inayoitwa "ulinzi wa watu" ilikuwa imefikiria kumtumia fulana ya kuzuia risasi na mlinzi. Lakini walichelewa. Carlos aliuawa siku ya Ijumaa.

Huko Puerto Wilches, kama ilivyo katika sehemu nyingi za nchi, magenge ya wahalifu, wapiganaji wa msituni na wanamgambo wanagombea udhibiti wa eneo hilo na wakazi. Makundi haya yote yenye silaha ambayo yanaishi kutokana na biashara ya madawa ya kulevya mara kwa mara yanafanya kazi kwa ushirikiano wa jeshi na polisi. Tangu kutawazwa kwa Gustavo Petro, viongozi saba wa mashrika ya kiraia wameuawa.

Rais mpya anajua kwamba kuna dharura. Hatua kadhaa zimetangazwa. Maafisa wa polisi na wanajeshi sasa watapoteza pointi na masuala mengine ya kikazi ikiwa uhalifu utafanywa katika maeneo wanayomiliki. Hii ni mbinu mpya ya usalama.

Mabadiliko kwenye uongozi wa jeshi

Na sera hii mpya ya usalama ilianza Agosti 12, siku tano baada ya kutawazwa kwa mkuu mpya wa nchi. Siku hiyo, Gustavo Petro, rais wa kwanza wa mrengo wa kushoto nchini Colombia, alibadilisha kamandi nzima ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na polisi, akisisitiza kwamba dhamira yake itakuwa "kupunguza ghasia, uhalifu, na ongezeko kubwa la heshima kwa haki za binadamu na uhuru”.

Alimteua Jenerali Helder Fernan Giraldo kama kamanda mkuu, na akamteua Jenerali Henry Armando Sanabria kama mkuu wa polisi, chini ya mamlaka ya Wizara ya Ulinzi, na ambayo Gustavo Petro tayari ameahidi "mabadiliko makubwa" na kifungu chake chini ya huduma mpya ya usimamizi. Kwa uteuzi huu, nguvu mpya ya kushoto imesababisha kuondoka kwa majenerali thelathini kutoka kwa jeshi na polisi, tukio ambalo halijawahi kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.