Pata taarifa kuu

Mzigo wa magonjwa yasiyoambukizwa waendelea kuwapa taabu wanawake wengi

Wanawake wanaotokea nchi zinazoendelea wanalazimika kubeba mzigo mkubwa wa kuwa walezi wa watu kwenye jamii wanaougua magonjwa yasiyoambukizwa ambayo husababisha vifo vya watu milioni 41 duniani kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Magonjwa haya ni kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu, kiharusi na magonjwa ya moyo.
Magonjwa haya ni kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu, kiharusi na magonjwa ya moyo. AP - Shelby Lum
Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwaka 2030, asilimia 74 ya vifo duniani vitakuwa vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza, asilmia zaidi ya sabini vikichangiwa na mataifa yanayoendelea.

Idadi hii kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa haya, inawalazimu wanawake wengi kuwa walezi.

Jenniffer Birir kutoka kaunti ya Bomet amekuwa akihudumia mgonjwa wa kisukari.

Kwake gharama ya chakula maalum, matunzo spesheli yameendelea kuathiri kazi yake ya ualimu na namna anavyoihudumia familia yake.

“ Wakati huu  chakula kama unga maalum wa wimbi ni bei juu ,haupatikani kwa urahisi na kila wakati inabidi uwe mbio mbio kumhudumia mgonjwa pamoja na watoto wako wanaohitaji kwenda shule kila siku,” alisikitika mama Jenniffer.

Naye Samantha Onyanzwa akitokea kaunti ya Butere, anaelezea masaibu yake kabla mamake mzazi kufariki kutokana na kisukari na shinikizo la damu.

“ Tumezaliwa na mandugu wa kiume lakini linapokuja swala la kuhudumia mama ,mara nyingi ilibidi mimi niache shughuli zangu ,na ndivyo ilivyo kwa sasa ,watoto wa kiume wanatuachia majukumu ya kuwalea wazazi.” alisema Samantha.

Getrude Mbeyu muuguzi wa wagonjwa wa saratani Pwani ya Kenya, anasema kupunguza mzigo huu, sharti serikali za Afrika kuwekeza katika taasisi za kuwatunza wagonjwa wanaougua kwa muda mrefu.

Magonjwa haya ni kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu,kiharusi na magonjwa ya moyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.