Pata taarifa kuu

Sheria ya Uingereza kuwatuma wahamiaji Rwanda haiendani na haki za nchi

Nairobi – Sheria ya serikali ya Uingereza kufufua mpango wake wenye utata wa kupeleka wahamiaji nchini Rwanda "haiendani" na wajibu wa haki za nchi hiyo, imesema ripoti ya jopo la waangalizi wa bunge la Uingereza.

Iwapo mswada huo utapitishwa, na mabunge yote mawili, wahamiaji haramu nchini Uingereza watasafirishwa nchini Rwanda
Iwapo mswada huo utapitishwa, na mabunge yote mawili, wahamiaji haramu nchini Uingereza watasafirishwa nchini Rwanda © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wabunge kwenye Kamati hiyo ya pamoja kuhusu haki za binadamu, wametoa kauli hiyo siku ya Jumatatu, baada ya kuupitia tena mswada huo ambao upo mbele ya bunge la juu kwa mjadala zaidi.

Katika ripoti yake ya kurasa, 52 Kamati hiyo imesema, pendekezo la mswada huo kuwa na kipengele cha kuzuia wahamiaji hao kwenda Mahakamani kupinga kupelekwa nchini Rwanda, haiendani kabisa na jukumu la Kimataifa la  Uingereza kuheshimu haki za binadamu.

Mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini DRC umekuwa ukikabiliwa na pingamizi
Mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini DRC umekuwa ukikabiliwa na pingamizi AFP - MARIA UNGER

Aidha, Kamati hiyo inayoundwa na wabunge watano wa chama tawala cha Conservative, imeonya kuwa iwapo mswada huo utapitishwa namna ulivyo, utakiuka utamaduni wa Uingereza wa kutoa uhuru kwa watu kulalamikia ukiukwaji wa haki zao.

Serikali ya Waziri Mkuu Rishi Sunak mwishoni mwa mwaka uliopita, iliwasilisha mswada huo tata baada ya Mahakama ya Juu kuamua kuwa, kuwatuma wahamiaji nchini Rwanda, ingekuwa kinyume cha sheria za Kimataifa.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu.
Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu. © Getty Images

Iwapo mswada huo utapitishwa, na mabunge yote mawili, wahamiaji haramu nchini Uingereza watasafirishwa nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.