Pata taarifa kuu

Somaliland inaishutumu Somalia kwa kuzuia ufikiaji wa anga yake

Mamlaka ya eneo lililojitangaza kujitenga la Somaliland imeshutumu serikali ya Somalia siku ya Alhamisi kwa "kupuuza" ahadi zake, hasa juu ya ufikiaji wa anga yake, katika muktadha wa mvutano unaoongezeka baada ya makubaliano kati ya jimbo hili la Somalia lililotangaza uhuru wake na Ethiopia.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) imetangaza kwamba imerudisha nyuma ndege mbili zilizokuwa zikielekea Somaliland.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) imetangaza kwamba imerudisha nyuma ndege mbili zilizokuwa zikielekea Somaliland. © Photo (Twitter/ Ethiopian Airlines)
Matangazo ya kibiashara

 

Serikali ya Mogadishu inapinga "itifaki ya mkataba" uliotiwa saini Januari 1 kati ya serikali ya Ethiopia na Somaliland inayotoa nafasi ya kukodisha kwa miaka 50 kwa Addis Ababa kilomita 20 ya ukanda wa pwani katika eneo hili ambalo lilitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991 na hautambuliwi na jumuiya ya kimataifa.

Serikali ya Somalia imeahidi kupambana kwa "njia zote za kisheria" dhidi ya nakala hii ambayo ni "uchokozi" wa Ethiopia na "ukiukwaji wa wazi" wa uhuru wake. Katika taarifa siku ya Alhamisi, mamlaka ya Somaliland imeishutumu kwa "kukataa kwa makusudi mikataba yote iliyohitimishwa" nao. "Serikali ya Somaliland inaitaka jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba mikataba hii, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa anga, (...) inaheshimiwa kwa njia isiyo na upendeleo na ya usawa," taarifa hiyo imeongeza.

Shutuma hizi zinakuja baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) kutangaza kwamba imerudisha nyuma ndege mbili zilizokuwa zikielekea Somaliland. Siku ya Jumatano, ilidai kuwa "ilikataa kuingia katika anga ya Jamhuri ya Somalia" kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia "iliyokuwa ikielekea Hargeisa", mji mkuu wa Somaliland, "baada ya kuthibitisha kuwa ndege hiyo haikuwa na idhini rasmi ya kutumia anga ya Somalia.

Kulingana na tovuti ya Flightradar, ndege hii yenye chapa ET8372 iliyoondoka Addis Ababa ilizunguka muda mfupi kabla ya mpaka wa Somalia na kurudi katika mji mkuu wa Ethiopia. Shirika la la kitaifa la Ethiopia, ambalo linasimamia safari za mara kwa mara na Hargeisa, haikujibu maombi ya shirika la habari la AFP kuhusu tukio hili. Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu abiria waliokuwa kwenye ndege hii.

Siku ya Alhamisi, SCAA imetangaza kwamba ilifanya vivyo hivyo kwa ndege ya mizigo "iliyosajiliwa Thailand" ambayo ilipaa kutoka Falme za Kiarabu, kwa sababu "imeshindwa kutoa maelezo ya shehena iliyokuwa imebeba".

Maudhui kamili ya "itifaki ya mkataba" iliyotiwa saini Januari 1 hayajawahi kuwekwa hadharani, lakini inaamsha wasiwasi wa nchi nyingi na mashirika ya kimataifa (Marekani, China, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Umoja wa Kiarabu. ..) ambao walitoa wito wa kuheshimiwa kwa uhuru wa Somalia. Addis Ababa inadai kwamba mkataba huo utaiwezesha kunufaika na kambi ya wanamaji na "huduma za kibiashara za baharini" kwenye Ghuba ya Aden.

Mamlaka ya Somaliland imehakikisha kwamba kwa kubadilishana, Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua rasmi kama taifa. Serikali ya Ethiopia imesema kwamba "itafanya tathmini ya kina kwa nia ya kuchukua msimamo kuhusu juhudi za Somaliland kupata kutambuliwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.