Pata taarifa kuu

Somalia yataka kufutwa kwa makubaliano ya Ethiopia/Somaliland kabla ya upatanishi wowote

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imejitenga katika taarifa mnamo Januari 18, 2024 kwa upatanishi wowote hadi Ethiopia itakapofuta makubaliano yaliyohitimishwa hivi majuzi na eneo linalojitenga la Somaliland, ambalo mamlaka ya Somalia inayachukulia kuwa "kinyume cha sheria".

Bandari ya Berbera huko Somaliland ndio kiini cha makubaliano kati ya Ethiopia na jamhuri hii ndogo iliyojitenga. (picha ya kielelezo)
Bandari ya Berbera huko Somaliland ndio kiini cha makubaliano kati ya Ethiopia na jamhuri hii ndogo iliyojitenga. (picha ya kielelezo) AFP - ED RAM
Matangazo ya kibiashara

Mvutano umekuwa mkubwa kati ya nchi hizo mbili jirani tangu makubaliano kati ya Addis Ababa na Somaliland, yalitekelezwa na kutiwa saini Januari 1 mkataba unaoikodishia hasa Ethiopia sehemu ya kilomita 20 kwenye ufuo wa Somaliland.

 

Serikali ya Somalia siku ya Alhamisi ilifutilia mbali upatanishi wowote na Ethiopia hadi itakapofuta makubaliano yaliyohitimishwa hivi majuzi na eneo linalojitenga la Somaliland, ambalo Mogadishu inachukulia hau hiyo kama "kinyume cha sheria".

Somaliland, eneo dogo la watu milioni 4.5 lililoko katika Ghuba ya Aden, ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991, lakini haukutambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Somalia inabaini kwamba makubaliano ya Januari 1 yanakiuka mamlaka yake ya ardhi, na inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono.

"Hakuna nafasi ya upatanishi mpaka pale Ethiopia itajiondoa kwenye hati hii haramu ya maelewano na kuthibitisha tena uhuru na uadilifu wa Somalia," wizara ya mambo ya nje ya Somalia imesema katika taarifa iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumatano, Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika lilitoa wito kwa Ethiopia na Somalia "kujizuia" wakati wa mkutano uliojadili suala hili. Siku ya Alhamisi, Jumuiya ya kikanda ya Afrika Mashariki ya IGAD ilisema inapanga kufanya mkutano usio wa kawaida nchini Uganda kuhusu suala hilo.

Tangu makubaliano yao, mamlaka ya Ethiopia na Somaliland zimetoa kauli zinazokinzana juu ya uwezekano wa kutambuliwa rasmi na Addis Ababa uhuru wa eneo lililojitenga.

Nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na wakaazi milioni 120, Ethiopia isiyo na bahari imedai katika miezi ya hivi karibuni kwamba inataka kupata tena Bahari Nyekundu, ambayo ilipoteza polepole na uhuru wa Eritrea mnamo mwaka 1993 na kuunganishwa katika miaka ya 1950, kisha mzozo na Asmara ulianza mnamo mwaka 1998 hadi 2000. Sehemu kubwa ya uagizaji wake na mauzo ya nje ya baharini sasa hupitia bandari ya Djibouti.

Somaliland inaendelea kuwa maskini licha ya eneo lake la kimkakati kwenye ufuo wa kusini wa Ghuba ya Aden, kwenye mojawapo ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za biashara duniani, kwenye lango la Mlango-Bahari wa Bab-el-Mandeb unaoelekea Bahari Nyekundu na mfereji kutoka Suez.

Somaliland iliingia katika makubaliano mwaka wa 2018 na DP World kwa ajili ya usimamizi wa bandari ya Berbera, katika uboreshaji wa kisasa ambao kampuni kubwa ya usimamizi wa bandari ya Emirati inawekeza mamilioni ya dola. Ethiopia ni sehemu ya makubaliano haya, ambayo yanaipa 19% ya hisa za bandari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.