Pata taarifa kuu

Wakuu wa IGAD kujadili mzozo katika nchi za Pembe ya Afrika

Nairobi – Wakuu wa nchi za IGAD, watakutana siku ya Alhamisi jijini Kampala nchini Uganda, kujadili mizozo kati ya nchi za pembe ya Afrika, ukiwemo mvutano kati ya Somalia na Ethiopia, iliyoingia kwenye makubaliano ya kijeshi na matumizi ya Bahari na Somaliland.

Wakuu wa nchi za IGAD
Wakuu wa nchi za IGAD © IGAD
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu utafanyika baada ya Somalia, kusema mkataba ulioingiwa kati ya Ethiopia na jimbo lililojitenga la Somaliland, linaingia uhuru wa nchi yake.

Mkataba huo unairuhusu Ethiopia kutumia baharí ya Shamu na kujenga kambi yake ya kijeshi katika jimbo la Somaliland ambalo lilitengaza kujitenga na Somalia tangu miaka ya tisini, lakini Somalia inakataa uhuru wa jimbo hilo.

Hali hii imezua hali ya wasiwasi kati ya Ethiopia na Somalia, huku rais Hassan Sheikh Mohammud akiifananisha serikali ya Ethiopia kama kundi la Al Shabab, na kuelezea kitendo chake kama cha kigaidi.

Eneo la Somaliland halijatambuliwa kimataifa kama nchi huru
Eneo la Somaliland halijatambuliwa kimataifa kama nchi huru © RFI

Katika hatua nyingine, Mkuu wa masuala ya diplomasia ya Somaliand Essa Kayd, ameitaka serikali ya Addis Ababa kulitambua jimbo hilo kama nchi huru, ili kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa.

Licha ya Somaliland kujitangazia uhuru wake, haitambuliwi na Jumuiya ya Kimataufa, inayofia kuwa, iwapo jimbo hilo litakuwa huru, maeneo mengine kwenye pembe ya Afrika yatataka kujitawala na hivyo kutikisa ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.