Pata taarifa kuu

DRC: Mfumuko wa bei, mojawapo ya kero kuu za wapiga kura

Hili ni mojawapo ya maswala makuu ya wapiga kura nchini DRC kabla ya uchaguzi wa Desemba 20: gharama kubwa ya maisha. Wakongo wanakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei.

Mfanyabiashara anayebadilisha fedha za kigeni katika mitaa ya Lubumbashi, DRC.
Mfanyabiashara anayebadilisha fedha za kigeni katika mitaa ya Lubumbashi, DRC. © Samir Tounsi / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Tamasha la sauti za watu wenye hasira katika uwanja wa Martyrs dhidi ya kupanda kwa dola. Tukio hilo limejirudia mara mbili katika miezi ya hivi karibuni. Kwanza mwishoni mwa mwezi wa Julai, Christophe Lutundula alipozungumza, wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Francophonie. Na mwishoni mwa mwezi wa Novemba, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi ya Félix Tshisekedi. Wasiwasi wa raia ambao rais anayemaliza muda wake lazima akumbane nao katika karibu kila hatua ya kampeni yake.

Wiki hii pekee, Benki Kuu iliripoti mfumuko wa bei ulioongezeka kwa 2.3% (33% kwa mwaka). Hali hii kwa kiasi fulani inatokana na kushuka kwa thamani ya faranga ya Kongo dhidi ya dola. Katika mwaka mmoja, sarafu ya taifa imepoteza zaidi ya 20% ya thamani yake dhidi ya dola (Faranga za Kongo za 2000 (FC) ziliuzwa dola moja mwezi Desemba 2022, 2675 FC kwa dola 1 mnamo Desemba 2023).

Kulingana na serikali, hali hiyo inaelezewa kimsingi na mambo ya nje, kuanzia na matokeo ya janga la Uviko-19 na athari za vita vya Ukraine. Waziri wa Fedha pia anataja tofauti za bei za malighafi, hususan kushuka kwa kasi kwa bei ya kobalti, ambayo ilishuka kutoka dola 81,000 hadi dola 31,000 kwa tani kati ya mwezi Machi 2022 na mwezi Machi 2023.

Kwa ndani, Kinshasa italazika pia kukabiliana na gharama kubwa, ili kufadhili mchakato wa uchaguzi au vita mashariki mwa nchi dhidi ya M23.

Kulingana na baadhi ya wataalam, wingi wa fedha katika mzunguko katika kipindi hiki cha uchaguzi inaweza pia kuwa na jukumu katika hili kupanda kwa dola. Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, Waziri Mkuu pia aliwataka wajumbe wa serikali inayohusika na masuala ya fedha, usambazaji wa mafuta na bidhaa nyingine muhimu kuendelea kuwa macho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.