Pata taarifa kuu

DRC: Raia Mashariki mwa nchi wanahisi kutelekezwa uchaguzi ukikaribia

Mashariki mwa DRC, kambi za wakimbizi katika eneo hilo ni ishara tosha kuwa serikali haijafanikiwa kutatua suala la usalama, wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi wa baadaye mwezi huu na raia wanahisi kutengwa.

Moja ya kambi ya wakimbizi Mashariki mwa DRC.
Moja ya kambi ya wakimbizi Mashariki mwa DRC. © Chube Ngorombi- RFI
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa raia wanahisi kutengwa, baadhi yao wakisema wanaishi kama wanyama, wengine wakidai hawakujisajili kwa ajili ya uchaguzi unaokuja huku wengine wakitilia shaka shughuli hiyo itaendeleaje wakati wao wanaishi kama wakimbizi.

Maeneo mengi ya Mashariki ni kitovu cha makundi yenye silaha  ambayo yamesababisha hali ya kibinadamu kuendelea kuwa mbaya, huku madaktari wasio na mipaka wakisema makumi kwa maelfu ya familia zinaendelea kutoroka mapigano jimboni Kivu Kaskazini.

Baadhi ya wagombea katika uchaguzi mkuu ujao wameahidi kukabiliana na utovu wa usalama katika eneo hilo ikiwa watachaguliwa, rais Felix Tshisekedi ambaye anawania kwa muhula wa pili akisema iwapo hajasuluhisha tatizo la usalama basi bado hajatimiza jukumu lake.

Kutokana na hali hii huenda raia katika baadhi ya maeneo ikiwemo himaya ya Masisi na Rutshuru, wakakosa kupiga kura kwa sababu ya uwepo kwa kundi la M23 ambalo linaendeleza mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.