Pata taarifa kuu

DRC: Wanasiasa waonywa dhidi ya kuchochea chuki na ukabila

Wiki mbili Baada ya Kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika tarehe 20 mwezi Desemba huko DRC, taasisi mbali mbali za kimataifa zinazofuatilia uchaguzi kwenye mataifa ya Afrika, ikiwemo Symocel, zimeonya kuhusu kuenea kwa hotuba zinazchochea chuki za kikabila na ubaguzi nchini Humo.

Daniel Finnan
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari jijini Kinshasa, Taasisi yenye waangalizi wa kimataifa na kitaifa , Symocel, imeeleza wasiwasi wake kufuatia kile inachosema kuenea kwa kampeni za chuki dhidi ya baadhi ya wagombea, hali ambayo inaweza kuzusha vurugu baina ya makabila. 

Katika kipndi hiki cha kampeni kumeshuhudiwa baadhi ya wagombea urais wakitoa hotuba katika maeneo tofauti ya nchi, bila ya kutajana majina wamekuwa wakihoji kuhusu uraia wa wengine, na hata kuwataja wengine kuwa wagombea wa wageni, lugha ambazo zimeanza kuzidisha mivutano baina ya makabila.

Vyombo vya habari vinasema ghasia ziliripotiwa, katika majimbo ya Haut-Katanga, Bandundu, Kindu na Kinshasa eneo la Limeté, Huko Haut-Katanga, mvutano ulizuka kati ya jamii ya Kasai na wakazi wa eneo la Kasumbalesa mwishoni mwa mwezi Novemba.

Symocel imetoa wito kwa wanasiasa wa DRC kuvumiliana na kufanya kampeni zao kistaarabu, ili kudumisha amani nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.