Pata taarifa kuu

Raia wa Sudan waandamana kuadhimisha mwaka 1 wa mapinduzi ya kijeshi

Polisi wamerusha mabomu ya machozi Jumanne kwa maelfu ya Wasudan ambao waliingia mitaani kuadhimisha mwaka wa mmoja wa mapinduzi na kutaka kuwepo na serikali ya kiraia, wakati mamlaka imezima intaneti na kutuma wanajeshi wengi kudhibiti waandamanaji.

Maandamano ya awali mjini Khartoum, Sudan, tarehe 10 Februari 2022.
Maandamano ya awali mjini Khartoum, Sudan, tarehe 10 Februari 2022. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

"Wanajeshi waende kambini," umeimba umati wa watu huko Khartoum na vitongoji vyake, ambapo barabara zote zilikuwa zimefungwa.

Waandamanaji waliweka vizuizi ili kupunguza kasi ya vikosi vya usalama, ambao walifunga madaraja na barabara kadhaa ili kuzuia kuongezeka kwa waandamanaji kuelekea ikulu ya rais Abdel Fattah al-Burhane, kiongozi mkuu wa mapinduzi ya Oktoba 25, 2021.

Tangu siku hiyo, waandamanaji na wanaharakati wamekuwa wakirejelea kauli mbiu hiyo hiyo: "hakuna mazungumzo au ushirikiano na viongozo wa mapinduzi" na raia kurejea madarakani,  kuanza tena kwa misaada ya kimataifa iliyositishwa kufuatia mapinduzi hayo.

Maafisa wa polisi walifyatua vitoa machozi katika jaribio la kutawanya umati wa watu, mashuhuda wamesema.

Mwaka mmoja uliopita, Jenerali Burhane, mkuu wa jeshi, alivunja ahadi zote zilizotolewa miaka miwili kabla nchini Sudan, nchi ambayo ilitumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Na misaada ya kimataifa inahitajika sana katika nchi hii, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani na ambapo hali ya kiuchumi ni mbaya.

Kati ya mfumuko wa bei wa tarakimu tatu na uhaba wa chakula, thuluthi moja ya wakazi milioni 45 wanakabiliwa na njaa. Hii ni 50% zaidi ya mwaka mmoja uliopita, limebaini shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Bei ya kikapu cha chini cha chakula imeongezeka kwa 137% katika mwaka mmoja, na kulazimu karibu kaya zote "kutumia zaidi ya theluthi mbili ya mapato yao kwa chakula", inaongeza WFP.

Mbali na hali ngumu ya maisha, Wasudan wengi wana wasiwasi, miaka mitatu baada ya "mapinduzi" ya 2019, kuhusu kurejea kwa udikteta wa kijeshi.

Kwa sababu tangu kuwekwa madarakani, waumini kadhaa wa Bw. Bashir, ambaye leo yuko gerezani, wamerejeshwa nyadhifa zao, hasa katika Mahakama ambayo kwa sasa inashughulikia kesi ya rais wa zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.