Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 130 waangamia kufuatia mafuriko yanayosababishwa na mvua Sudan

Watu 134 wamepoteza maisha nchini Sudan baada ya kusombwa na maji kufuatia mafuriko makubwa yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. 

Ongezeko la vifo limeripotiwa, kutoka watu 112 mapema mwezi huu hadi 134, huku jimbo la Kordofan Kaskazini likiongoza kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.
Ongezeko la vifo limeripotiwa, kutoka watu 112 mapema mwezi huu hadi 134, huku jimbo la Kordofan Kaskazini likiongoza kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo. Ebrahim Hamid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza la kijeshi nchini humo linasema mbali na watu hao kupoteza maisha, wengine 120 wamejeruhiwa lakini pia makaazi  ya watu yameharibiwa, ikiwemo mimea ya wakulima mashambani. 

Nyumba ambazo zimeharibiwa na mafuruko, zinakadiriwa kuwa zaidi ya 128,000 na tayari serikali imetangaza hali ya dharura katika majimbo 18 ya nchi hiyo. 

Ongezeko la vifo limeripotiwa, kutoka watu 112 mapema mwezi huu hadi 134, huku jimbo la Kordofan Kaskazini likiongoza kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo. 

Majimbo mengine yaliyoathiriwa na mafuriko hayo ni pampka na Gedaref , Kassala na Darfur ambalo pia Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto UNICEF likisema nalo, limeathiriwa zaidi. 

Umoja wa Mataifa unahofia kuwa, kufikia mwisho wa mwaka huu huenda watu 460,000 wakaathiriwa na mafuriko hayo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.