Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Kiongozi wa serikali ya Sudan hatakuwa mgombea katika uchaguzi ujao

Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, anayetawala Sudan baada ya mapinduzi ya kijshi karibu mwaka mmoja uliopita, alisema siku ya Alhamisi hatashiriki katika chaguzi zijazo, ambazo zitaweka serikali inayoongozwa na raia.

Jenerali Al-Burhane wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021.
Jenerali Al-Burhane wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021. © REUTERS/Sarah Meyssonnier/Pool/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Sina hamu ya kuwania kama mgombea," Jenerali Burhane, 62, alisema katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

Sudan imekuwa katika machafuko kwa zaidi ya miaka mitatu. Uchumi wake unadorora na, kulingana na Shirika la Fedha Duniani, mfumuko wa bei unatarajiwa kufikia asilimia 245 mwaka huu.

Tangu mapinduzi ya Oktoba mwaka jana, waandamanaji wanaounga mkono demokrasia wameendelea kuandamana mitaani wakitaka majenerali wakabidhi madaraka kwa raia.

Wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji mara kadhaa na kuwaua baadhi yao na kuwaweka kizuizini mamia. Ingawa hakuna afisa wa polisi au afisa wa vikosi vya usalama ambaye amehukumiwa kwa vifo hivyo, Jenerali Burhane alisema watu watano au sita wanachunguzwa. "Waandamanaji walipambana na polisi, na polisi waliwashughulikia kwa mujibu wa sheria kulinda mali ya umma," alisema.

Jenerali huyo, hata hivyo, aligoma kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi ujao, ingawa hapo awali alitangaza kwamba uchaguzi unaweza kufanyika mwezi wa Julai 2023. Anaona kuwa mgogoro huo uko katika ngazi ya wahusika wa kisiasa ambao lazima wakubaliane kuhusu tarehe ya uchaguzi. Alisisitiza kuwa jeshi halina nafasi katika mjadala huu.

Pia alipuuzilia mbali uvumi kuhusu mvutano ndani ya serikali yake ya mpito, akikana kuwepo kwa kutofautiana na naibu mkuu wa baraza la kijeshi tawala la Sudan, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kwa jina la utani la Hamedti. Katika wiki za hivi karibuni, vyombo vya habari nchini Sudan viliripoti mzozo kati ya majenerali hao wawili. Hivi majuzi Hamedti alikiri kwamba unyakuzi wa kijeshi haukufaulu.

Msaada wa Marekani 'umesitishwa'

Mamilioni ya Wasudan wanateseka chini ya uzani wa mfumuko wa bei na sarafu, fedha ya Sudan, ambayo thamani yake imeshuka kwa kiasi kikubwa dhidi ya dola ya Marekani.

Mkuu huyo wa kijeshi anayetawala alishutumu nchi na taasisi ambazo hakuzitaja kuwa ndizo zinazochangia kuzorota kwa hali ya kiuchumi ya Sudan.

Kufuatia mapinduzi hayo, utawala wa Biden ulisimamisha msaada wa kifedha wa dola milioni 700 uliokusudiwa kusaidia kipindi cha mpito kuelekea serikali ya raia wote. Wizara ya Mambo ya Nje ilisema mpango mzima wa msaada, ambao ungeweza kujumuisha usaidizi wa ziada juu ya dola milioni 700, ulikuwa umesimamishwa kusubiri mapitio ya Marekani kuhusu hali ya Khartoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.