Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

Makabiliano mabaya yatokea katika Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga

Mtu mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa siku ya Jumatano wakati askari wa kulinda mazingira walipovamiwa na "kundi la wavamizi" katika Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira ya Kongo (ICCN) imesema.

Walinzi wa Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga wakishika doria katika eneo karibu na Volkano ya Nyiragongo mnamo Mei 28.
Walinzi wa Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga wakishika doria katika eneo karibu na Volkano ya Nyiragongo mnamo Mei 28. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Walinzi hao, waliokuwa wakishika doria kaskazini mwa mbuga hiyo, huko Kasindi/Lubiliha, karibu na mpaka wa Uganda, "walishambuliwa kikatili kwa mapanga (...) na umati wa wavamizi waliokuwa wamebebelea mapanga", imesema ICCN katika taarifa. "Kiongozi wa kikosi cha askari hao alijeruhiwa vibaya na silaha yake kuchukuliwa na wavamizi", taarifa imebainisha. Hata hivyo walinzi wengine walipata silaha hiyo na, "katika mazingira haya ya kujihami, watu wawili walipigwa kwa bahati mbaya, mmoja wao alifariki dunia kutokana na majeraha," ICCN imeongeza.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ICCN inasema inalaani "mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya wafanyakazi wake katika eneo hili", ikitoa wito kwa "mahakam kutoa mwanga kamili juu ya tukio hili" na "raia kuwa watulivu na kuweka mbele mazungumzo". Migogoro inayohusiana na mipaka ya hifadhi hutokea mara kwa mara katika sekta hii, hasa kwa wakulima wanaoishi kutokana na shughuli ya kilimo.

Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, ambayo ni kubwa na pana mashariki mwa DRC kwenye mipaka ya Rwanda na Uganda, inasifika kwa sokwe wa milimani na volkano, lakini pia imejaa makundi ya watu wenye silaha kwa miaka mingi. ICCN ni shirika la umma ambalo linasimamia makumi ya mbuga na hifadhi nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.