Pata taarifa kuu

Mkuu wa operesheni za jeshi la Kongo dhidi ya M23 akamatwa

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kamanda wa operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la waasi la "M23" mashariki mwa nchi hiyo, amekamatwa na kufungwa jela, vyombo vya habari vya Kongo vimetangaza siku ya Jumanne, vikibaini kwamba anashtumiwa "uhaini wa hali juu."

Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyombo hivi vya habari, ambavyo vinanukuu ndugu wa Luteni Jenerali Philémon Yav Irung na "vyanzo vya usalama", afisa huyu anafungwa tangu Jumatatu jioni huko Makala, gereza kuu la Kinshasa.

Chanzo cha kijeshi kimelithibitishia shirika la habari la AFP, kwa sharti la kutotajwa jina, kukamatwa kwa Luteni Jenerali Yav, bila maelezo yoyote juu ya sababu inayowezekana ya kukamatwa kwake. Akiulizwa kuhusu kukamatwa kwa afisaa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la DRC, Jenerali Léon-Richard Kasonga, msemaji wa majeshi ya DRC (FARDC), hakutaka kujibu.

Kamanda wakanda ya tatu ya ulinzi, ambayo inajumuisha eneo lote la mashariki na kaskazini mashariki mwa DRC, Philémon Yav alichukua usimamizi wa operesheni za kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini dhidi ya M23 katikati ya mwezi wa Julai. Alikuwa amechukua nafasi ya Jenerali Constant Ndima, gavana wa kijeshi wa mkoa huo.

Kundi la M23, la "Movement of March 23", ni kundi la waasi wa zamani wengi wao kutoka kabila la Watutsi lililoshindwa mwaka wa 2013, ambalo lilichukua silaha tena mwishoni mwa mwaka jana, likiishutumu Kinshasa kwa kutoheshimu makubaliano kuhusu kuwarejesha baadhi ya wapiganaji wake katika maisha ya kiraia na kuwaingiza wengine katika vikosi vya ulinzi na usalama. DRC inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi hili la waasi, madai ambayo Kigali inakanusha.

Kwa muda wa miezi mitatu, waasi wa M23 wameshikilia mji wa Bunagana, eneo muhimu katika eneo la Rutshuru, kwenye mpaka wa Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.