Pata taarifa kuu

DRC: Hali bado si shwari Maï-Ndome

Nchini DRC, hali bado ni ya wasiwasi huko Maï-Ndome, mji ambao umeendelea kukumbwa na ghasia kikabila tangu mwanzoni mwa mwezi wa Agosti mwaka huu. 

Gari la MSF mbele ya kituo cha matibabu nchini DRC.
Gari la MSF mbele ya kituo cha matibabu nchini DRC. AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashirika ya kiraia, karibu watu wanne wameuawa katika eneo hilo, karibu na Bandundu. Mgogoro huu pia umesababisha watu kadhaa kujeruhiwa na watu wengi kuyatoroka makazi yao. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ndilo shirika pekee la kibinadamu lililopo katika eneo hili kaskazini mashariki mwa Kinshasa.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linasema limetoa zaidi ya huduma matibabu 750 pamoja na msaada wa kisaikolojia kwa watu waliopatwa na kiwewe, likiweka mbele shughuli zake za kliniki, kuwekwa vyoo, usambazaji wa dharura wa maji na chakula na usafirishaji wa majeruhi.

Shirika hilo lisilo la kiserikali pia linabainisha kuwa katika mkoa wa Kwamouth, watu waliotoroka makazi yao wameanza kurejea makwao, vurugu zimehamia mashariki na eneo la Bandundu. Alessandra Giudiceandrea, mkuu wa ujumbe wa MSF nchini DRC anasema "Kwa hakika ni jibu kwa wimbi hili la majeruhi bila kupuuza msaada wa majeraha ambayo watu wamepitia. Katika maeneo ambayo kulikuwa na shambulio mnamo mwezi wa Agosti, watu wanarudi makwao polepole. Lakini kote katika barabara hiyo, kuna mashambulizi ambayo yanaendelea kwenye vijiji vingine. Wacha tuseme jiografia ya mivutano inaonekana kubadilika."

Afisa huyo anaongeza kuwa hali bado ni ya wasiwasi na kwamba MSF inaendelea na shughuli zake huko Maï-Ndombe, na hasa katika eneo la Kwamouth.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.