Pata taarifa kuu

Waasi wa Tigray wanaishutumu Addis Ababa kwa kuanzisha mashambulizi ya pamoja na Eritrea

Nchini Ethiopia, kundi la waasi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) sasa linaituhumu Addis Ababa kwa kuanzisha mashambulizi ya pamoja na Eritrea. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Eritrea kuhusika moja kwa moja tangu mapigano yalipoanza tena tarehe 24 Agosti.

Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wakibebwa na lori kwenye barabara moja karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia Mei 8, 2021.
Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wakibebwa na lori kwenye barabara moja karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia Mei 8, 2021. © Ben Curtis/AP
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa kijeshi wa TPLF anashutumu vikosi vya Ethiopia na Eritrea kwa kuanzisha "vita vya kila namna dhidi ya Tigray". Anasema mashambulizi hayo yalianzishwa usiku, karibu 4:30 alfajiri. Majeshi hayo mawili yaliripotiwa kushambulia kutoka Eritrea kwa pande nne katika eneo la Adiyabo kaskazini magharibi mwa Tigray, anasema Getachew Reda, msemaji wa TPLF.

Serikali ya Ethiopia haijajibu tuhuma hii. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Alhamisi hii asubuhi, Addis Ababa imeridhika kuthibitisha kwamba jeshi lake linafanya kazi katika hali ya kujihami, dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Tigray ambayo yameongezeka. Vyanzo vya kidiplomasia vinathibitisha kwamba hivi karibuni wameona idadi kubwa ya askari kwenye mpaka huu kati ya Tigray na Eritrea.

Eritra tayari imechukua jukumu kubwa katika vita hivi, ilichangia hasa katika mashambulio ambayo yaliwezesha jeshi la Ethiopia karibu miaka miwili iliyopita kurejesha Tigray kwenye himaya yao, hata kama Abiy Ahmed, Waziri Mkuu, alisubiri hadi Mei 2021 kukiri uwepo wa wanajeshi wa Eritrea katika ardhi ya Ethiopia.

Wanajeshi hawa wa Eritrea pia wanashutumiwa kwa kufanya dhuluma nyingi. Kurudi kwao kwenye ardhi ya Ethiopia kutajumuisha ongezeko lingine kubwa katika kiwango cha vita hivi vilivyoanza tena siku nane zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.