Pata taarifa kuu

Ethiopia: Waasi wa Tigray waanzisha mashambulizi kuelekea kusini wakati mapigano yakizidi

Mapigano yanaendelea kusini mwa nchi ya Ethiopia. Siku ya Jumamosi jeshi la shirikisho lilitangaza kuwa limejiondoa kutoka Kobo, eneo ambalo si mbali na mpaka na Tigray na kuangukia mikononi mwa waasi. Tangu wakati huo, mapigano yameripotiwa kuelekea mji wa kimkakati wa Weldiya, katika mkoa wa Amhara.

Wanajeshi wa Jeshi la Kitaifa la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) wakiandamana katika mitaa ya Kombolcha, Ethiopia tarehe 11 Desemba 2021.
Wanajeshi wa Jeshi la Kitaifa la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) wakiandamana katika mitaa ya Kombolcha, Ethiopia tarehe 11 Desemba 2021. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kutoka mashirika ya misaada ya kibinadamu na mashahidi waliripoti mapigano ya Jumatatu katikati ya eneo la Kobo na mji wa Weldiya, ulioko takriban kilomita hamsini kusini mwa jimbo la Amhara na kuchukuliwa kuwa njia muhimu. Barabara hii inawawezesha waasi wa Tigray kufungua njia inayoelekea mji mkuu Addis Ababa kusini na barabara inayoelekea katikati mwa jimbo la Amhara. Shahidi kutoka Kobo, aliyehamia Weldiya, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba alisikia milio mingi ya risasi siku ya Jumatatu na kubaini kwamba kunaripotiwa "mapigano makali ambayo karibu" na eneo hilo, ameripoti mwandishi wetu katika ukanda huo, Florence Morice.

Vyanzo vichache vyakutoka eneo hilo vinataja makabiliano makali na raia wakitoroka makazi yao kufuatia mapigano hayo. Vikosi vya waasi vinadai kuzima mashambulizi ya serikali iliyoanzisha kuelekea mji mkuu wao, Mekele.

'Kuzima' vitisho vya usalama Tigray

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Getachew Reda, msemaji wa kundi la waasi la TPLF, alikaribisha wanajeshi wake kufanikiwa "kukabiliana na" "uchokozi" ulioanzishwa na Addis Ababa dhidi ya Tigray, amesema. Ameapa kuwa vikosi vyao "vitaendelea kusonga mbele", akithibitisha kwamba lengo la "mashambulizi" ya TPLF sio "kudhibiti" maeneo mapya katika eneo la Amhara, lakini "kuangamiza" mtu yeyote. atayetishia usalama wa jimbo la Tigray.

Tunapozungumza, sehemu kubwa ya Wollo ya kaskazini iko mikononi mwetu. Hatuna nia maalum ya kudhibiti eneo hili au lile. Lakini maadamu majeshi ambayo yatuandama yanaendelea kutishia usalama wa raia wetu, tutaendelea kuchukua hatua stahiki kuondosha tishio hilo. Iwapo kugeuza tishio hili kutatupeleka sehemu za Amhara au jimbo la Afar ni suala jingine. Lakini inaonekana kama hatuwezi kutegemea jumuiya ya kimataifa kumdhibiti Abiy Ahmed na vibaraka wake wa vita kwa ajili ya usalama wetu, ni wazi. Ni lazima tutegemee nguvu zetu wenyewe, sio tu kupunguza tishio, lakini pia kulinda dhidi ya vitisho sawa, iwe vinatoka Kaskazini, Mashariki, Magharibi au Kusini, haijalishi.

Msemaji wa mamlaka ya Tigray, Getachew Reda anasema vikosi vya TPLF 'vitaendelea kuchukua hatua zinazofaa kupunguza' tishio lolote huko Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.