Pata taarifa kuu

Ethiopia: Hospitali ya Mekele yalengwa na mashambulizi mapya

Vurugu zimeongezeka nchini Ethiopia, wiki moja baada ya kuanza tena kwa mapigano. Mji mkuu wa Tigray, Mekele, umelengwa tena na mashambulizi ya anga usiku kucha. Mamlaka katika jimbo la Tigray imeshutumu jeshi la Ethiopia, ambalo halikujibu.

Gari la wagonjwa la shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) likiwasili katika Hospitali Kuu ya Mekele, ambayo imelendwa na mashambulizi ya angani.
Gari la wagonjwa la shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) likiwasili katika Hospitali Kuu ya Mekele, ambayo imelendwa na mashambulizi ya angani. © YASUYOSHI CHIBA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa hospitali ya Ayder ndiye ambaye alitoa tahadhari hiyo jana usiku kwa kushutumu shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya Mekele muda mfupi kabla ya saa sita usiku. "Waathiriwa wanafika hospitalini", ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kulingana na msemaji wa waasi wa TPLF, mabomu matatu yalirushwa na hospitali ya Mekele ilikuwa miongoni mwa walengwa, ameshutumu. Vyanzo vingine vya ndani vinahakikisha kwamba baadhi ya majengo ya hospitali hii yameathirika, lakini hali halisi ya malengo na uharibifu bado ni vigumu kubaini asubuhi hii. TPLF inahakikisha kwa vyovyote vile kwamba ngome au kambi za kijeshi hazijalengwa katika mashambulizi haya mapya katika eneo hilo, kwani baada ya shambulio la bomu katika shule ya chekechea huko Mekele wiki iliyopita, jeshi la Ethiopia lilikuwa limehakikisha kwamba lilikuwa linalenga kambi za kijeshi tu.

Dalili nyingine ya kuongezeka kwa uhasama, serikali inawatuhumu waasi wa Tigray kwa kuanzisha tena mashambulizi kuelekea mpaka na Sudan ambako mapigano yanasemekana kuendelea. Wakati tangu mwanzoni mwa wiki hii, TPLF imeendelea nje ya mipaka ya Tigray, huko Amhara kuelekea mji muhimu wa Weldiya, pamoja na eneo la Afar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.