Pata taarifa kuu
LIBYA-SUDANI-Mapigano-Ugaidi-Usalama

Libya: Ansar Al Sheria yawekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi

Umoja wa Mataifa umeliweka kundi la Ansar Al Sheria kwenye orodha ya makundi ya kigaidi. Umoja wa Mataifa unalituhumu kundi hilo kutekeleza vitendo vya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya Libya.

Wanajeshi wa Libya akiwafyatulia risase wapoiganaji wa Ansar al Sheria, Novemba 25 mwaka 2013 katika mji waBenghazi.
Wanajeshi wa Libya akiwafyatulia risase wapoiganaji wa Ansar al Sheria, Novemba 25 mwaka 2013 katika mji waBenghazi. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Libya imeendelea kushuhudia mapigano kati ya jeshi na makundi ya wapiganaji wa kiislam tangu ulipoangushwa utawala wa Moamar Al Kadhafi.

Ansar Al Sheria imeendelea kunyooshewa kidole kwa kutekeleza mauaji katika maeneo mbalimbali ya Libya.

Wakati huohuo Ufaransa imebaini kwamba utawatuma wanajeshi wake kusaidia kijeshi serikali ya Libya kwa lengo la kuyatokomeza makundi ya kigaidi. Wanajeshi wa Ufaransa wanajiandaa kuingia katika ardhi ya Libya wakipitia kaskazini mwa nchi hiyo.

Awali Libya ilioumba Umoja wa Mataifa kuisaidia kijeshi baada ya kuonekana kushindwa kukabiliana na makundi ya wapiganaji wa kiislam, ambao wamedhibiti baadhi ya maeneo muhimu nchini humo.

Serikali ya Libya imekua ikiituhumu Sudani kufadhili makundi ya wapiganaji wa kiislam yanayoendelea kuhatarisha usalama katika baadhi ya maeneo ya Libya.

Libya imeendelea kushuhudia mdororo wa kiusalama tangu ulipoangushwa utawala wa Moamar Al Kadhafi, ambao wengi waliona kuwa utawala huo ni wa kimla.

Hivi karibuni makundi ya wapiganaji wa kiislam yameyateka baadhi ya maeneo muhimu ukiwemo mji mkuu wa Lbya, Tripoli.

Marekani na Libya zinalichukulia kundi la Ansar Al Sheria miongoni mwa makundi ya kigaidi ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.