Pata taarifa kuu
LIBYA-SUDAN-Usalama-Mapigano

Serikali ya Libya yainyooshea kidole Sudan

Serikali halali ya Libya imeishutumu serikali ya Sudani kuwasaidia kijeshi wanamgambo walioko mjini Tripoli na kumuomba mwambata wa kijeshi wa Ubalozi wa Sudani nchini Libya kuondoka nchini humo.

Mapigano kati ya makundi yenye silaha katika eneo la Qaqaa, katika mji wa Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014.
Mapigano kati ya makundi yenye silaha katika eneo la Qaqaa, katika mji wa Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Serikali hiyo iliyoko mafichoni eneo la Tobruk baada ya mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha jijini Tripoli imesimamisha ndege moja mjini Kufra na kubaini kuwa ndege hiyo ilikuwa ya Sudan ikibeba vifaa vya kijeshi kwa ajili ya wanamgambo walioko jijini Tripoli.

Serikali ya Libya imegundua kwamba ndege aina ya Antonov ya Sudani ilikuwa ikielekea mjini Tripoli na kuituhumu serikali ya Khartoum kusambaza silaha kwa wapinzani wao ambao kwao ni "magaidi". Ndege hiyo imegunduliwa katika eneo la Kufra katika jangwa kusini-mashariki.

Ndege ikiharibiwa kutokana na mapigano yaliyojitokeza katika uwanja wa Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014.
Ndege ikiharibiwa kutokana na mapigano yaliyojitokeza katika uwanja wa Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014. REUTERS/Aimen Elsahli

Kwa upande wake, serikali ya Sudan imejitetea kwa kusema kwamba silaha hizo ni kwa ajili ya operesheni ya pamoja baini ya Sudan na Libya kwa minajili ya kupiga doria mpakani, utetezi ambao serikali ya Libya imetupilia mbali hasa baada ya ziara ya aliyekuwa spika wa Bunge nchini Libya ambapo wabunge wengi walikuwa wanaongoza harakati za Kiislam na kutaka serikali mbadala.

Sakata hili linaweka bayana shutuma za viongozi halali wa Libya za kuwepo kwa uhusiano wa karibu baina ya serikali ya Sudan na tawi la Muslim Brotherhood nchini Libya likizungumzia msaada huo kama "haramu" na kumtaka mwambata wa kijeshi wa Sudana nchini Libya kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.